An-Noor
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَخْشَ ٱللَّهَ وَيَتَّقْهِ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَآئِزُونَ 52
{52} Alipotaja fadhila ya utiifu katika kuhukumu hasa; ametaja fadhila zake kwa ujumla katika hali zote, na akasema: “Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake,'' na akasadikisha habari yao na akatii amri yao, "na wakamwogopa Mwenyezi Mungu;" yaani, kumuogopa hofu iliyo pamoja na elimu ya kumjua, na akaacha aliyoyakataza nayo, na akaiepusha nafsi yake na yale anayoyatamani. Na kwa ajili hiyo amesema, ''na wakamcha Mwenyezi Mungu;'' kwa kuacha haramu; kwa sababu uchamungu kwa ujumla ni pamoja na kufanya yale yaliyoamrishwa na kuacha yale yaliyoharamishwa, na pale yanapokutanishwa na wema na utiifu. Kama ilivyo katika hali hii, inafasiriwa kuwa ni kuepuka adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuacha maasi yake. ''Basi hao;'' waliojumuisha utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na utiifu kwa Mtume wake, na hofu ya Mwenyezi Mungu, na uchamungu wake, ''ndio wenye kufuzu'' kwa kuepushwa kwao na adhabu; kwa kuacha kwao sababu zake; na kufika kwao kwenye malipo; kwa kutenda kwao sababu zake; kwani kufaulu kumezuiliwa kwao wao, na ama yule asiyesifika kwa sifa zao; hakika kutampita yeye kufaulu kulingana na mapungufu yake kutokamana na sifa hizi nzuri. Aya hii ilijumuisha haki ya pamoja kati ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo ni utiifu unaotakiwa kwa ajili ya imani, na haki mahsusi kwa Mwenyezi Mungu, nayo ni hofu na uchamungu. Na imebakia haki ya tatu mahsusi kwa Mtume, nayo ni kumsaidia na kumheshimu; kama alivyozichanganya haki tatu katika Sura Al-Fath katika kauli yake: ''Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumheshimu, na mumtakase asubuhi na jioni.''