Al-Baqara
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّآ أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَا۟ ٱلَّذِى بِيَدِهِۦ عُقْدَةُ ٱلنِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوٓا۟ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا۟ ٱلْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ 237
{237} Yani mkiwataliki wanawake kabla ya kuwagusa, na baada ya kuwakatia mahari maalumu, basi wanawake hao waliotalikiwa wana nusu ya mahari iliyokatwa, nanyi mna nusu yake. Hilo ndilo la wajibu, maadamu halijaingiliwa na kusamahe na kutupilia mbali, kwa namna kwamba mwanamke amsamehe mumewe nusu yake hiyo ikiwa msamaha wake ni sahihi. "Au amesamehe yule ambaye fundo la ndoa liko mkononi mwake" naye ni mume kulingana na rai iliyo sahihi. Kwa sababu, yeye ndiye ambaye mkononi mwake kuna kufungua fundo lake. Na kwa sababu msimamizi (wa mwanamke) si sahihi kwa kusamehe kile ambacho ni haki ya mwanamke, kwa sababu yeye si mmiliki (wa hilo) wala wakili (wa mwanamke). Na ilisemwa: Huyo ni baba, naye ndiye ambaye matamshi ya Aya hii tukufu yanaashiria. Kisha akahimiza kusamehe, na kwamba mwenye kusamehe, anakuwa karibu zaidi na kumcha Mungu. Kwa sababu ni wema unaolazimu kufunguka kwa kifua, na kwa sababu mtu hatakiwi kuipuuza nafsi yake katika suala la hisani na wema. Na anasahau fadhila ambazo ndizo daraja la juu zaidi za kuamiliana. Kwa sababu, kuamiliana na watu baina yao kwa wao kuna daraja mbili: Ima uadilifu ulio wajibu. Nao ni kuchukua kilicho wajibu na kupeana kilicho wajibu. Na ima fadhila na hisani. Nao ni kupeana kisicho wajibu, na kuwa rahisi wa kuamiliana katika haki zake, na kutoangalia yale yaliyomo ndani ya nafsi yake. Hivyo basi, mtu hafai kusahau daraja hii, angalau katika baadhi ya nyakati. Hasa kwa yule ambaye kati yako na yeye kuna kuamiliana au kuchanganyika. Kwani Mwenyezi Mungu huwalipa wafanyao wema kwa fadhila na ukarimu. Na ndiyo maana akasema, "hakika, Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda." Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: