Al-Baqara
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
فَمَنۢ بَدَّلَهُۥ بَعْدَ مَا سَمِعَهُۥ فَإِنَّمَآ إِثْمُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ 181 فَمَنْ خَافَ مِن مُّوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 182
Na kwa kuwa mwenye kuusia anaweza kukataa kuusia, kwa sababu ya anachodhania kwamba wale wa baada yake anaweza badili aliyoyausia, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
{181 - 182} “Na atakayeibadilisha,” yani wasia kwa waliotajwa au wengineo “baada ya kuusikia” [yani] baada ya kuufahamu. Na akazijua njia zake na kuutekeleza kwake, "basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoibadilisha." Vinginevyo, aliyeusia malipo yake tayari yamekwisha fika kwa Mwenyezi Mungu, lakini dhambi ni juu ya mwenye kubadilisha, mwenye kughairi. “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia.” Yeye husikia sauti zote, pamoja na kusikia kwake maneno ya mwenye kuusia na wasia wake. Kwa hivyo, inampasa amchunge yule anayemsikia na kumuona, na wala asifanye dhuluma katika wasia wake. “Mwenye kujua” nia yake na anayajua matendo ya aliyeusiwa. Basi mwenye kuusia akijitahidi, na Mwenyezi Mungu akajua hilo katika nia yake, atamlipa hata ikiwa atakosea. Na ndani yake kuna onyo kwa yule anayeusiwa dhidi ya kubadilisha. Kwani Mwenyezi Mungu anamjua (alieyusiwa), na anaona anayofanya, basi na amtahadhari Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo hukumu ya wasia yenye uadilifu. Na ama wasia ambayo ina dhuluma ndani yake na kwenda kombo, na dhambi, basi inampasa anayemhudhuria mwenye kuusia wakati wa wasia kumshauri kwa lililo bora zaidi na lenye uadilifu; na kwamba amkataze dhidi ya dhuluma na kwenda kombo. Nako ni kule kwenda kombo katika wasia bila ya kukusudia. Nalo dhambi ni kukusudia kufanya hivyo.Na asipofanya hivyo, basi inampasa (mwenye kusuluhisha) kusuluhisha baina ya waliousiwa, na afikie uadilifu baina yao kwa msingi wa kuridhiana na kusuluhishana, na kuwausia kuiondolea dhima (lawama) maiti wao. Basi mwenye kufanya hivyo, atakuwa amefanya wema mkubwa, na hakuna dhambi juu yao, kama ilivyo dhambi juu ya aliyebadilisha wasia. Na ndio maana akasema: “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Msamehevu.” Yani Yeye husamehe makosa yote, na hutupilia mbali yale yanayotokana na hayo kwa mwenye kutubu kwake. Na pia inaingia hapo msamaha wake kwa mwenye kujikasirikia na kumwachia ndugu yake baadhi ya haki zake. Kwa sababu anayesamehe, Mwenyezi Mungu humsamehe, na ni Msamehevu kwa maiti wao aliyefanya dhuluma katika wasia wake; ikiwa watatarajia malipo (kwa Mwenyezi Mungu) kwa kusameheana wao kwa wao kwa ajili kuitoa dhima yake (maiti) katika lawama. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye rehema kwa waja wake, ambapo aliwawekea sheria ya kila amri ambayo kwayo wanarehemeana na kuhurumiana. Basi aya hizi zikaonyesha kuhimizwa kufanya wasia, na kubainisha ni kwa nani, na tishio la adhabu kwa mwenye kuibadilisha wasia yenye uadilifu, na kuhimiza kusuluhisha wasia yenye dhuluma.