Al-Baqara
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
قُلْ أَتُحَآجُّونَنَا فِى ٱللَّهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ وَلَنَآ أَعْمَـٰلُنَا وَلَكُمْ أَعْمَـٰلُكُمْ وَنَحْنُ لَهُۥ مُخْلِصُونَ 139
(139) Kuhojiana ni majadiliano baina ya watu wawili au zaidi kunakohusiana na masuala yenye utata, kiasi kwamba, kila mmoja wa wapinzani hao wawili anataka kuunga mkono kauli yake na kubatilisha kauli ya mpinzani wake. Hivyo basi, kila mmoja wao anajitahidi katika kusimamisha hoja juu ya hilo. Na linalotakiwa katika kuhojiana ni kwamba kuwe kwa yaliyo mema kwa njia ya karibu zaidi ambayo mpotevu anaweza kurudishwa katika haki. Na inasimamisha hoja juu ya mkaidi, na inaweka wazi haki na inabainisha batili. Na majadiliano yakitoka nje ya mambo haya, basi yanakuwa kubishana na kugombana kusikokuwa na heri ndani yake, na kunakoleta uovu kiasi kunavyoleta. Na watu wa kitabu walikuwa wanadai kwamba wao ndio wanaomstahiki zaidi Mwenyezi Mungu kuliko Waislamu. Na haya ni madai tu ambayo hayana dalili na ushahidi. Ikiwa Mola Mlezi wa watu wote ni mmoja, basi (yeye) siyo Mola Mlezi wenu tu na siyo sisi, na kila mmoja kati yetu na nyinyi ana matendo yake, basi sisi na nyinyi tunakuwa sawa katika hilo. Na hilo halilazimu kwamba moja ya makundi haya mawili limstahiki zaidi Mwenyezi Mungu kuliko lingine. Kwa sababu, kutenganisha katika vitu vinavyoshirikina katika jambo bila ya tofauti yenye kuathiri ni madai ya uwongo, na kutenganisha baina ya vitu vinavyofanana na kiburi cha dhahiri. Lakini ubora hupatikana kwa kumsafishia Mwenyezi Mungu matendo mema. Na hali ni sifa ya waumini peke yao. Kwa hivyo, ikabakia tu kwamba wao ndio wanaomstahili zaidi Mwenyezi Mungu kuliko wengine, kwa sababu kumsafishia Mwenyezi Mungu matendo ndiyo njia ya wokovu. Hii ndiyo tofauti baina ya marafiki wa Ar-rahman (Mwingi wa Rehema) na marafiki wa Shetani kwa sifa za kweli, ambazo watu wenye akili wanazikubali na wala hapingani katika hilo isipokuwa kila mwenye jeuri, mjinga. Kwa hivyo, katika aya hii, upo mwongozo mzuri mno wa njia ya kuhojiana, na kwamba mambo yamejengeka juu ya kuleta pamoja yale yanayofanana, na kutenganisha baina yale yaliyo tofauti.