Al-Israa
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَإِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فِى ٱلْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّآ إِيَّاهُ ۖ فَلَمَّا نَجَّىٰكُمْ إِلَى ٱلْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ ٱلْإِنسَـٰنُ كَفُورًا 67
{67} Na miongoni mwa rehema zake zinazoashiria kuwa Yeye pekee ndiye anayeabudiwa na si mwingine ni kwamba yakiwapata madhara baharini, na wakahofu kuangamia kwa sababu ya kurundikana kwa mawimbi, wanatoweka wale ambao wao walikuwa wakiwaomba kama vile walio hai na wafu, badala ya Mwenyezi Mungu wakiwa katika nyakati nzuri. Na ni kana kwamba hawakuwahi kuwaomba wakati wowote ule, kwa kuwa walijua kwamba wao ni dhaifu na hawawezi kuondoa madhara, hivyo wakapiga kelele wakimuomba Muumba wa ardhi na mbingu, ambaye viumbe vyote vinamtafuta msaada katika shida zao, na wakamsafishia yeye tu dua na kumnyenyekea katika hali hii. Basi pindi Mwenyezi Mungu alipowaondolea madhara hayo na akawaokoa na wakawa katika nchi kavu, wakasahau yale waliyokuwa wakiyaomba kabla, na wakamshirikisha na wale wasionufaisha, wala hawadhuru, wala hawapeani, wala hawanyimi, na wakaacha kumsafishia matendo Mola wao Mlezi na Mfalme wao. Na haya ni katika ujinga wa mtu na ukafiri wake. Kwa maana mtu ni mwenye kukufuru sana neema isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, basi akamneemesha akili timamu na akaongoka kwenye njia iliyonyooka. Yeye, anajua kwamba mwenye kuondosha dhiki na kuokoa kutokana na mambo ya kutisha ndiye anayestahiki kupwekeshwa, na kumsafishia yeye tu matendo katia dhiki, faraja, wepesi na ugumu. Na ama aliyeachiliwa mbali, na akaachwa kusimamiwa na akili dhaifu, yeye hakuona katika wakati wa dhiki isipokuwa manufaa yake ya sasa na kuokoka kutoka katika hali hiyo yote, na pindi alipookoka na shida hiyo ikamuondoka, akadhani kwa ujinga wake kwamba amemshinda Mwenyezi Mungu, na wala haikumjia katika akili yake matokeo yoyote ya kidunia, sembuse mambo ya akhera.