Yusuf
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَلَمَّا فَتَحُوا۟ مَتَـٰعَهُمْ وَجَدُوا۟ بِضَـٰعَتَهُمْ رُدَّتْ إِلَيْهِمْ ۖ قَالُوا۟ يَـٰٓأَبَانَا مَا نَبْغِى ۖ هَـٰذِهِۦ بِضَـٰعَتُنَا رُدَّتْ إِلَيْنَا ۖ وَنَمِيرُ أَهْلَنَا وَنَحْفَظُ أَخَانَا وَنَزْدَادُ كَيْلَ بَعِيرٍ ۖ ذَٰلِكَ كَيْلٌ يَسِيرٌ 65
65. Basi “walipofungua mizigo yao, wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa” Huu ni ushahidi kwamba walikuwa wanajua kuwa Yusuf aliwarudishia kwa makusudi, na kwamba alitaka kuwapa hizo bidhaa kama mali. Kwa hivyo, wakamwambia baba yao wakimhimiza amuachilie ndugu yao pamoja nao: "Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi?” Yaani, tutake kitu gani baada ya ukarimu huu mzuri, kwani alitupimia kwa ukamilifu na akaturudishia bidhaa zetu kwa njia [hii] njema inayojumuisha ikhlasi na maadili mema? "Hizi bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee watu wetu chakula.” Yaani: tukienda na ndugu yetu, itakuwa ni sababu ya yeye kutupimia, na tutawajia watu wetu na chakula kikuu wanchohitaji sana, "na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia” kwa kumuachilia aende pamoja nasi. Kwani yeye humpimia kila mtu shehena ya ngamia mmoja. “Na hicho ni kipimo kidogo.” Yaani, ni kipimo chepesi ambacho hakikudhuru. Kwa maana muda hautakuwa mrefu, na masilahi tayari yameshabainika.