सीधे कंटेंट पर जाएँ
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
सूरह 2

Al-Baqara

यह तफ़सीर अस-सअदी का एक अनुवाद है, जैसा IslamHouse.com उसे saadi.islamenc.com पर प्रकाशित करता है, उस साइट के पन्नों से लिया गया। साइट यह नहीं बताती कि इसका अनुवाद किसने किया या यह किस छपे संस्करण का अनुसरण करता है, और इसका पाठ लेने की कोई शर्तें नहीं बताती, इसलिए इसे दिखाने का अधिकार सत्यापित नहीं है। किसी ने इसे छपी किताब से नहीं मिलाया है और किसी आलिम ने इसकी समीक्षा नहीं की है। हर अंश उन आयतों के पास है जिन पर वह टिप्पणी करता है; वे आयतें Tanzil का क़ुरआनी पाठ हैं, जैसा वहाँ है; जिस आयत की साइट अपनी अलग टिप्पणी नहीं देती वह अपने से पहले के अंश के साथ रहती है, और सूची ऐसी हर आयत का नाम देती है। सबील ने इसमें से कुछ भी न लिखा है, न अनुवाद किया है।

पाठ का स्रोत:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 को लिया गया

आयतें 280–281

وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا۟ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ 280 وَٱتَّقُوا۟ يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى ٱللَّهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ 281

{280-281} "Na (mdaiwa) akiwa ni mwenye ugumu, basi (mdai) ampe muhula mpaka awe katika wepesi." Yani ikiwa anayedaiwa deni yuko katika hali ngumu, na hawezi kulilipa, basi inamlazimu mdai wake kumpa muda hadi apate wepesi. Naye inamlazimu akipata njia yoyote ile ya kulipa inayoruhusika kwamba alipe anachodaiwa. Na ikiwa mdai wake atampa sadaka kwa kulitupilia mbali deni lote au sehemu yake, basi hilo ni heri kwake. Na inamrahisishia mja kushikamana na mambo ya kisheria, na kuepuka miamala ya riba. Na kuwafanyia wema wale wenye ugumu akijua kwamba atakuwa na siku ambayo ndani yake atarejea kwa Mwenyezi Mungu. Na atamlipa matendo yake, na hatamdhulumu uzito wa chembe, kama alivyohitimisha Aya hii kwa kauli yake. "Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilichochuma. Nao hawatadhulumiwa." Kisha Mola Mtukufu akasema: