सीधे कंटेंट पर जाएँ
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
सूरह 2

Al-Baqara

यह तफ़सीर अस-सअदी का एक अनुवाद है, जैसा IslamHouse.com उसे saadi.islamenc.com पर प्रकाशित करता है, उस साइट के पन्नों से लिया गया। साइट यह नहीं बताती कि इसका अनुवाद किसने किया या यह किस छपे संस्करण का अनुसरण करता है, और इसका पाठ लेने की कोई शर्तें नहीं बताती, इसलिए इसे दिखाने का अधिकार सत्यापित नहीं है। किसी ने इसे छपी किताब से नहीं मिलाया है और किसी आलिम ने इसकी समीक्षा नहीं की है। हर अंश उन आयतों के पास है जिन पर वह टिप्पणी करता है; वे आयतें Tanzil का क़ुरआनी पाठ हैं, जैसा वहाँ है; जिस आयत की साइट अपनी अलग टिप्पणी नहीं देती वह अपने से पहले के अंश के साथ रहती है, और सूची ऐसी हर आयत का नाम देती है। सबील ने इसमें से कुछ भी न लिखा है, न अनुवाद किया है।

पाठ का स्रोत:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 को लिया गया

आयत 129

رَبَّنَا وَٱبْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ 129

(129) "Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee kati yao," yani katika kizazi chetu "Mtume anaye tokana na wao" ili liwe la kuinua zaidi daraja zao; na ili waweze kumfuata, na ili wamjue hakika ya kumjua. "Awasomee Aya zako" kwa maneno, kuhifadhi, na kuhifadhisha "na awafundishe Kitabu na hekima" kimaana "na awatakase." Kwa kuwalea juu ya matendo mema, na kuwa mbali na matendo maovu ambayo nafsi hazitakasiki pamoja nayo. "Hakika Wewe, ndiye Mwenye nguvu," yani mwenye nguvu za kushinda kila kitu, ambaye hakiizuii nguvu zake chochote "Mwenye hekima." Ambaye huweka vitu pahali pake. Basi kwa Nguvu zako na hekima yako, mtume huyu mtume kati yao. Mwenyezi Mungu akawaitikia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamtuma Mtume huyu mtukufu ambaye kupitia kwake Mwenyezi Mungu aliirehemu dhuria yao wawili hasa, na viumbe vingine vyote kwa ujumla. Na kwa sababu hiyo, akasema, rehema na amani ziwe juu yake, “Mimi ni dua ya baba yangu Ibrahim."