Al-Burooj
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
قُتِلَ أَصْحَـٰبُ ٱلْأُخْدُودِ 4 ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلْوَقُودِ 5 إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ 6 وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ 7 وَمَا نَقَمُوا۟ مِنْهُمْ إِلَّآ أَن يُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ 8 ٱلَّذِى لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ 9
{4 - 9} "Wameangamizwa watu wa makhandaki." Nazo ni zile handaki zilizochombwa na hao watu ambao walikuwa makafiri waliokuwa wakiishi pamoja na watu Waumini, wakawahimiza waingie katika dini yao, lakini Waumini wakakataa kufanya hivyo, kwa hivyo makafiri hao wakachimba mahandaki katika ardhi, wakawasha humo moto, wakakaa pembezoni mwake, wakatia Waumini mtihanini kwa kuwaleta mbele ya moto huo. Basi yeyote aliyewaitikia wakawa wanamwachilia. Na anayeendelea kuamini, wakawa wanamtupa katika moto huo. Hiki ndicho kiwango kikubwa mno cha kupigana vita Mwenyezi Mungu na kundi lake la waumini, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawalaani, akawaangamiza na akawaahidi adhabu. Akasema: “Wameangamizwa watu wa makhandaki." Kisha akaeleza maana ya mahandaki hayo kwa kauli yake. "Yenye moto wenye kuni nyingi, walipokuwa wamekaa hapo. Na wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini." Hii ni miongoni mwa aina kubwa zaidi za kiburi na ugumu wa mioyo. Kwa sababu walichanganya kati ya kukufuru ishara za Mwenyezi Mungu, kuzifanyia ukaidi, kupigana vita na watu wake, na kuwatesa kwa adhabu hii ambayo nyoyo zinapasuka kwa sababu yake, na kuwepo kwao pamoja nao walipokuwa wanawatupa humo. Hali ni kuwa hawakuona baya lolote kwa Waumini ila kwa hali - wanayosifiwa kwa sababu yake na ambayo kwayo ndiyo wanaweza kuwa furahani, nayo ni kwamba walikuwa wamemuamini "Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa mno." Yaani, mwenye nguvu ambaye kwa hizo alishinda kila kitu, na anayesifiwa katika maneno yake, vitendo vyake na sifa zake. "Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi" kwa kuviumba viumbe, na kwamba wao ni waja wake ambao anawaendesha apendavyo. "Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu" kwa elimu yake, kusikia kwake na kuona kwake. Basi je, wale waliomuasi hawahofu kwamba Mwenye Nguvu na Mwenye uwezo anaweza kuwachukua kwa adhabu? Au hawakujua wote kwamba wao ni wamilikiwa wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mwenye mamlaka juu ya yeyote bila idhini ya Mmiliki wa kweli? Au imefichikana kwao kwamba Mwenyezi Mungu anayajua vyema matendo yao na atawalipa kwa hayo? Sivyo, hakika kafiri yuko katika udanganyifu, naye mjinga yuko katika upofu na upotevu mbali na njia iliyonyooka.