Al-Haaqqa
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
فَإِذَا نُفِخَ فِى ٱلصُّورِ نَفْخَةٌ وَٰحِدَةٌ 13 وَحُمِلَتِ ٱلْأَرْضُ وَٱلْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَٰحِدَةً 14 فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ ٱلْوَاقِعَةُ 15 وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِىَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ 16 وَٱلْمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرْجَآئِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَـٰنِيَةٌ 17 يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌ 18
{13 - 18} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja aliyowafanyia wale waliokadhibisha Mitume wake, na jinsi alivyowalipa, na akawaharakishia adhabu yao katika dunia, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaokoa Mitume na wafuasi wao, huu ukawa ni utangulizi wa malipo ya kiakhera na utimilifu wa matendo kamili Siku ya Kiyama. "Na litakapopulizwa barugumu mpulizo mmoja tu" - wakati miili itakapokuwa imeota kikamilifu - kwa mpulizo mmoja, hapo roho zitatoka, kisha kila roho itaingia ndani ya mwili wake. Na tazama, watu wote watakuwa tayari wamemsimamia Mola Mlezi wa walimwengu wote. "Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja." Yaani, hivyo vyote vitakuwa tambarare, uwanda. Hutaona humo mdidimio wala muinuko. Hivyo ndivyo itakavyofanywa ardhi na vyote vilivyo juu yake. Na ama mbingu, hizo zitafadhaika, kutikisika na kupasuka - na rangi yake itabadilika, na kuwa dhaifu kabisa baada ya uimara na nguvu zake kubwa, na hayo si kwa sababu ya lolote ila ni kwa sababu ya jambo kubwa lililozisumbua, na balaa kubwa mno iliyozidhoofisha mno. "Na malaika" watukufu "watakuwa pembezoni mwa mbingu" huku wamemnyenyekea Mola wao Mlezi, watiifu kwa ukuu wake; "na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi." Nao ni malaika wenye nguvu kubwa zaidi. Wakati atakapokuja kwa ajili ya kutenganisha kati ya waja na kuhukumu baina yao kwa uadilifu wake na fadhila zake, na ndiyo maana akasema: "Siku hiyo mtahudhurishwa" kwa Mwenyezi Mungu, "haitafichika siri yoyote yenu." Siyo katika miili yenu na dhati zenu wala katika vitendo vyenu na sifa zenu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua ya ghaibu na yanayoonekana. Na waja watakusanya bila viatu, uchi na bila ya kutahiriwa, kwenye ardhi tambarare ambayo ataweza kuwasikilizisha mwitaji, na ataweza kuwaona mtazamaji, na hapo atawalipa kwa yale waliyofanya, na ndiyo maana akataja namna yatakavyokuwa malipo hayo, akasema: