Aller au contenu
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sourate 6

Al-An'aam

Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.

Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22

Verset 94

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَٰدَىٰ كَمَا خَلَقْنَـٰكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَـٰكُمْ وَرَآءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَـٰٓؤُا۟ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ 94

94. Basi hii ndiyo hali yao katika Barzakh (kaburini). Na ama siku ya Qiyama, wao kwa hakika watakapoifikia hali ya kuwa ni wafilisi, wakiwa mmoja mmoja, bila ya familia, wala mali, wala wana, wala askari, wala wasaidizi. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyowaumba mara ya kwanza huku wakiwa hawana kila kitu. Kwani vitu huchukuliwa kama mali, na vinakuja baada ya hayo kupitia sababu zake ambazo ni sababu zake. Na katika siku hiyo yatakatika mambo yote ambayo yalikuwa pamoja na mja katika dunia isipokuwa matendo mema na matendo mabaya ambayo ndiyo uhakika wa Nyumba ya Akhera, ambayo yanatoka humo, na unakuwa uzuri wake, na ubaya wake, na furaha yake, na huzuni yake, na wasiwasi yake kubwa, na adhabu yake, na neema yake kulingana na matendo. Hayo ndiyo yenye kunufaisha au kudhuru, na kuwa mabaya au kufurahisha. na ama yasiykuwa hayo miongoni mwa familia, na wana, na mali, na wasaidizi, ni msaada tu wa kutoka nje, na sifa zenye kuondoka, na hali zenye kuzuia. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Nanyi hakika mmetujia mmoja mmoja kama tulivyowaumba mara ya kwanza. Na mkayaacha yote yale tuliyowapa." Yaani, tuliwapa na tukawaneemesha kwavyo "nyuma ya migongo yenu." Hayawafai kitu, "na wala hatuwaoni pamoja nanyi hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu." Kwa maana, washirikina wanamshirikisha Mwenyezi Mungu na wanaabudu pamoja naye Malaika, na Manabii, na wale walio wema na wasiokuwa hao. Nao hao wote ni wa Mwenyezi Mungu, lakini wanawafanyia viumbe hawa sehemu katika nafsi zao, na ushirika katika ibada zao. Na haya ni madai tu kutoka kwao na ni dhuluma. Kwa maana wote ni waja wa mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mmiliki wao na anayestahiki kuabudiwa. Basi ushirikina wao katika ibada, na kuwafanyia kwao baadhi ya waja ni kuwafanya hao kuwa katika daraja la Muumba, Mmiliki. Kwa hivyo watakemewa Siku ya Qiyama, na waambiwe maneno haya; "na wala hatuwaoni pamoja nanyi hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Hakika, yamekatika mahusiano baina yenu." Yaani, yalikatika mafungamano na njia zilizo baina yenu na washirika wenu, kama vile uombezi na mambo mengine, kwa hivyo hayakuwa na manufaa yoyote na hayakufanikisha chochote. "Na yamewapotea yale mliyokuwa mkidai" miongoni mwa faida, na amani, na furaha, na wokovu ambayo Shetani aliwapambia, na akayafanya kuwa mazuri katika nyoyo zenu; basi ndimi zenu zikayatamka, na mkadanganyika na madai haya batili, ambayo hayana uhakika wowote, wakati kilipowabainikia kinyume cha yale mliyokuwa mkidai. Na ikadhihirika kuwa nyinyi ndio wenye hasara kubwa kwa nafsi zenu, na ahali zenu, na mali zenu.