Al-An'aam
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ ٱلَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَٱلْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ ٱللَّهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ 36
Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake - "hakika wanoitikia" kulingania kwako, na kuukubali ujumbe wako, na wanafuata amri yako na makatazo yao ni "wale wanaosikia" kwa nyoyo zao yale ya kuwanufaisha, nao ni wale wenye akili na masikio. Na kinachokusudiwa na kusikia hapa ni kusikia kwa moyo na kuitikia; vinginevyo, kusikia kwa masikio tu wanashirikiana katika hilo mwema na muovu. Basi kila anayejukumishwa na sheria tayari hoja ya Mwenyezi Mungu Mtukufu imeshasimama juu yake kwa kusikia Aya zake, na hawakubaki na udhuru wowote wa kutokubali. "Na ama wafu, Mwenyezi Mungu atawafufua, kisha kwake Yeye ndiko watakakorejeshwa." Inawezekana kwamba maana yake ni kinyume cha maana iliyotajwa hapo juu; yaani, walio hai moyoni tu ndio wanaokuitikia. Ama wale waliokufa mioyoni mwao ambao hawaisikii furaha yao na wala hawahisi kitakachowaokoa; wao hawatakuitikia, wala hawatakufuata, na miadi yao ni siku ya Qiyama. Mwenyezi Mungu atawafufua, kisha kwake ndiko watakakorejeshwa. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa na Aya hii ni maana yake ya dhahiri, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasimulia uhakika wa kuwepo kwa Qiyama. Na kwamba atawafufua wafu Siku ya Kiyama, kisha atawapa habari juu ya yale waliyokuwa wakiyafanya. Na inakuwa katika hilo, kuhimiza kumuitikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na vitishio dhidi ya kutofanya hivyo.