Al-Maaida
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
إِنَّآ أَنزَلْنَا ٱلتَّوْرَىٰةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا ٱلنَّبِيُّونَ ٱلَّذِينَ أَسْلَمُوا۟ لِلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلرَّبَّـٰنِيُّونَ وَٱلْأَحْبَارُ بِمَا ٱسْتُحْفِظُوا۟ مِن كِتَـٰبِ ٱللَّهِ وَكَانُوا۟ عَلَيْهِ شُهَدَآءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا۟ ٱلنَّاسَ وَٱخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِى ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَـٰفِرُونَ 44
{44} "Hakika Sisi tuliiteremsha Taurati" kwa Musa bin Imran Rehema na Amani zimshukie. "Yenye uwongofu" wenye kuongoa kwenye Imani na haki, na inalinda dhidi ya upotovu "na nuru," iangazwayo kwayo katika giza la ujinga, na mchanganyiko, na shaka, na fikira potofu, na matamanio. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na hakika tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi, na mwangaza, na ukumbusho kwa wachamungu," "ambayo kwayo wanahukumu" - kati ya wale waliotubia na kurudi, yaani Mayahudi, katika masuala na fatwa. - "Manabii walionyenyekea kiislamu" kwa Mwenyezi Mungu na wakafuata amri zake, ambao Uislamu wao ni mkubwa zaidi kuliko Uislamu wa wengineo, na wao ndio wateule wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake. Basi ikiwa manabii hawa watukufu na mabwana wa wanadamu waliichukua kuwa kielelezo, na wakaifuata, na kutembea nyuma yake; basi ni nini kilichowazuia hawa walio duni miongoni mwa Wayahudi kuichukua kuwa kielelezo chao? Na ni nini kilichofanya kuacha jambo tukufu zaidi lililo ndani yake, yaani kumwamini Muhammad – Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, – ambaye hayakubaliwi matendo ya dhahiri na ya ndani isipokuwa kwa itikadi hiyo? Je, wana imamu katika jambo hili? Ndiyo, wanao maimamu ambao tabia yao ni kupotosha na kusimamisha uongozi wao na vyeo vyao baina ya watu na kula kwa kuficha haki na kudhihirisha batili. Hawa ndio maimamu wa upotovu ambao wanalingania kwenye Moto. Na kauli yake, "wachamungu, na wanazuoni wa kiyahudi," yaani, pia wanahukumu kwa Taurati juu ya Mayahudi maimamu wa dini miongoni mwa wachamungu. Yaani, wanachuoni wafanyao matendo na wafunzao, wanaowalea watu kwa malezi mazuri zaidi, na wanafuata pamoja nao njia ya Manabii wenye huruma. Na wanazuoni wa Kiyahudi, yaani, wanachuoni wakubwa ambao maneno yao huchukuliwa kuwa kielelezo, na matendo yao yanaheshimiwa, na wana ulimi mkweli katika umma zao. Na hukumu hiyo iliyotoka kwao yenye kuafikiana na haki ni, "kwa kuwa walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake." Yaani, ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kukihifadhi Kitabu chake, na akawafanya kuwa wadhamini juu yake, nacho ni amana kwao. Na akawawajibishia kukihifadhi kutokana na nyongeza, na kupunguza, na kuficha, na kukifunza kwa asiyekijua, nao ni mashahidi juu yake kwa namna kwamba wao ndio wanaorejelewa kuhusiana nacho katika yale yanayowachanganya watu humo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwabebesha watu wenye elimu kile ambacho hakuwabebesha wajinga. Kwa hivyo ni wajibu kwao kutekeleza mizigo ya yale waliyobebeshwa, na kwamba wasichukue kielelezo kutoka kwa wajinga kwa kukaa tu bila ya kazi na kufanya uvivu. Na kwamba wasitojitosheleze tu na ibada za mtu binafsi kama aina mbalimbali za utajo wa Mwenyezi Mungu, na Swala, na Zaka, na Hijja, na Saumu, na mfano wa hayo miongoni mwa mambo ambayo ikiwa watayafanya wale wasiokuwa watu wa elimu, watasalimika na kanusurika. Ama watu wa elimu; kama vile wanavyotakiwa kufanya yale ambayo wao wenyewe wanatakiwa kuyafanya, pia wanatakiwa kuwafundisha watu, na kuwatanabahisha juu ya yale wanayohitaji katika mambo ya dini yao. Hasa mambo ya kimsingi, na ambayo hutokea mara kwa mara, na kwamba wasiwaogope watu, bali wamuogope Mola wao Mlezi. Na ndiyo maana akasema, "Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache." Mkaificha haki, na mkaidhihirisha batili kwa ajili ya starehe chache za dunia. Basi maradhi haya ikiwa mwenye elimu atasalimika kutokana nayo, basi kwa kuwezeshwa kwake na furaha yake. Kwamba iwe hamu yake ni kujitahidi katika elimu na kufundisha, na anajua kwamba Mwenyezi Mungu alimwamuru kuhifadhi kile alichomkabidhi katika elimu na akamfanya kuwa shahidi juu yake. Na kwamba amhofu Mola wake Mlezi, wala hofu ya watu na kuwanyenyekea kusimzuie kufanya yale ambayo ni ya lazima kwake, na kwamba asiipendelee dunia kuliko dini. Kama vile alama ya upotovu wa mwenye elimu ni awe mwenye kuegemea kwa kukaa tu bila ya kutekeleza yale aliyoamrishwa. Wala kutojali yale aliyokabidhiwa kuhifadhi, akawa ameyaachilia na kuyapoteza, akawa ameiuza dini kwa dunia, akawa amepokea rushwa katika hukumu zake, na akachukua mali kwa fatwa zake, na wala hakuwafundisha waja wa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa malipo na kuwekewa kitu maalum. Basi huyu, Mwenyezi Mungu alimpa neema kubwa, akaikufuru, na akatupa fungu kubwa ambalo wasiokuwa yeye walinyimwa. Basi tunakuomba, Ewe Mola Mlezi, elimu yenye manufaa na matendo yenye kukubaliwa, na kwamba uturuzuku msamaha na kuwa salama kutokana na kila balaa, Ewe Mkarimu. "Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu," kama vile haki iliyo wazi, na akahukumu kwa batili ambayo anaijua kwa sababu ya lengo miongoni mwa malengo yake potovu. "Basi hao ndio makafiri." Kwa hivyo, kuhukumu kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu hakukiteremsha ni miongoni mwa vitendo vya watu wa kufuru. Na huenda ukawa ukafiri wa kumtoa katika dini, na hilo ikiwa ataitakidi uhalali wake na kuruhusika kwake. Na huenda likawa katika madhambi makubwa, na katika matendo ya ukafiri, ambayo mwenye kuyafanya anastahiki adhabu kali.