Al-Maaida
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْكُفْرِ مِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِأَفْوَٰهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ ۛ سَمَّـٰعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّـٰعُونَ لِقَوْمٍ ءَاخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ ٱلْكَلِمَ مِنۢ بَعْدِ مَوَاضِعِهِۦ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَٱحْذَرُوا۟ ۚ وَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ فِتْنَتَهُۥ فَلَن تَمْلِكَ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَمْ يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا خِزْىٌ ۖ وَلَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ 41
{41} Mtume-rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa kwa sababu ya wingi wa kuwajali viumbe, anamhuzunikia mwenye kudhihirisha imani kisha akarudi kwenye ukafiri. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamuelekeza kwamba asisikitike wala asihuzunike juu ya mfano wa hawa. Kwani, hawa hawako katika msafara wala katika jeshi. Wakihudhuria, hawanufaishi kitu. Na wasipokuwepo, hawatafutwi. Na kwa sababu hiyo akasema, akibainisha sababu inayofanya ya kutowahuzunikia, kwa hivyo akasema, "miongoni mwa wale waliosema kwa vinywa vyao, "Tumeamini", na hali nyoyo zao hazikuamini." Kwani wale wanaosikitikiwa na kuhuzunikiwa ni wale wanaohesabiwa miongoni mwa Waumini, nao ni Waumini kwa nje na ndani. Na Mwenyezi Mungu aepushe kwamba hawa waiache dini yao na waritadi. Kwa maana, imani inapochanganyika bashasha yake mioyo, basi mwenyewe hawezi kuifanya kuwa sawa na kinginecho, na wala hawezi kutafuta mbadala wake. "Na miongoni mwa wale waliotubia na kurudi kwa Mwenyezi Mungu" yaani, Mayahudi, "wanaosikiliza sana uongo, wanaowasikiliza sana kaumu wengine ambao hawajakujia." Yaani wanawaitikia na kuwaiga viongozi wao ambao mambo yao yamejengeka juu ya uwongo, na upotovu na makosa. Na viongozi hawa wanaofuatwa "hawajakujia" bali walikupa mgongo, na wakafurahia yale ya batili waliyo nayo. Nayo ni kupotosha maneno kutoka pahali pake panapofaa. Yaani, kuyapa maneno maana ambazo Mwenyezi Mungu hakuyataka wala hakuyakusudia ili kuwapotosha viumbe kwa ajili ya kuisukuma haki. Basi hawa wanaowatii hawa wanaolingania kwenye upotovu, wanaofuata yasiyowezekana, ambao wanakuja na kila uongo, hawana akili wala hima; pia, usijali ikiwa hawatakufuata. Kwa sababu wamepungukiwa sana, na kile kilichopungukiwa hakiangaliwi wala hakijaliwi. "Sema, "Mkipewa haya, basi yachukueni, na msipopewa haya, tahadharini." Yaani, hii ndiyo kauli yao wanapotaka kukufanya hakimu, na wala hawana nia isipokuwa kufuata matamanio yao. Wanaambiana wao kwa wao, ikiwa Muhammad atawahukumia kwa hukumu hii ambayo inakubaliana na matamanio yenu, basi ikubalini hukumu yake. Na asipowahukumia kwayo, basi jihadharini kufuata katika hilo. Ni hii ni fitna na kufuata yale yanayotamaniwa na nafsi. "Na yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumfitini, basi huwezi kuwa na uwezo kwa ajili yake mbele ya Mwenyezi Mungu." Kama kauli yake Yeye Mtukufu, "Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye." "Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu hataki kuzisafisha nyoyo zao." Yaani, ndiyo maana yalitokea kwao yale yaliyotokea. Hii likaashiria kuwa yule ambaye makusudio yake katika kutafuta hukumu ya kisheria ni kufuata matamanio yake, na kwamba akihukumu kwa ajili yake anaridhika, na asipohukumu kwa ajili yake, anakasirika. Kwa maana hilo ni katika ukosefu wa usafi wa moyo wake, na hilo linaashiria kwamba usafi wa moyo ni sababu ya kila heri; nao ndio sababu kubwa inayoitia kusema kila kauli iliyo ya busara, na matendo yaliyo sawasawa. "Wana hizaya katika dunia," yaani, fedheha na kuaibishwa. "Na Akhera wana adhabu kubwa," nayo ni Moto na hasira ya Al-Jabbar (Mwenye kufanya alitakalo).