An-Nisaa
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا۟ ٱلنِّسَآءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا۟ بِبَعْضِ مَآ ءَاتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّآ أَن يَأْتِينَ بِفَـٰحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰٓ أَن تَكْرَهُوا۟ شَيْـًٔا وَيَجْعَلَ ٱللَّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا 19
{19} Walikuwa katika Jahiliyyah akifa mmoja wao na kumwacha mkewe, jamaa yake kama vile kaka yake, na binamu yake, na mfano wao anaona kwamba yeye ndiye anayemstahiki zaidi mke wake kuliko kila mtu mwingine. Na akamzuia mke huyu dhidi ya mwingine yeyote, apende au achukie. Basi ikiwa atampenda, anamuoa kwa mahari anayoipenda mume huyu na si yeye. Na kama hakumridhia, anamzuia asimuoe isipokuwa yule amchaguaye yeye. Na labda angekataa kumuoza mpaka ampe kitu katika urithi wa jamaa yake au katika mahari yake. Na mwanamume pia alikuwa akimzuia mkewe ambaye yeye anamchukia ili amnyang’anye baadhi ya kile alichompa. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawakataza Waumini hali hizi zote isipokuwa hali mbili tu: Akiridhia na akachagua kuolewa na jamaa wa mume wake wa kwanza, kama inavyofahamika katika maana isipokuwa ya moja kwa moja katika kauli yake, "kwa lazima." Na wakifanya uchafu ulio dhahiri, kama vile uzinifu na maneno machafu, na kumdhuru mumewe. Basi katika hali hii, inaruhusika kwake kumzuia mkewe ili kumwadhibu kwa yale aliyoyafanya, ili aweze kujikomboa kutoka kwake ikiwa amemzuia kwa uadilifu. Kisha akasema, "Na kaeni nao kwa wema." Na hili linajumuisha kukaa nao kwa maneno na kwa matendo. Basi ni juu ya mume kuishi na mkewe kwa wema, kwa usuhuba mzuri, na kujiepusha kumdhuru, na kuwatendea ihsan na kuamiliana kwa uzuri. Na inaingia katika hilo pesa za matumizi na mavazi, na mfano wake. Basi ni wajibu kwa mume kumfanyia mkewe wema unaofaa kutoka kwa aliye mfano wake kwa mke aliye mfano wa mkewe katika wakati huo na pahali hapo. Na hili linatofautiana kulingana na hali. "Na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia heri nyingi ndani yake." Yani inafaa enyi waume muwashikilie wake zenu hata kama mnawachukia, kwa sababu kuna heri nyingi katika hilo. Katika hilo, ni kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na kukubali wasia wake, ambao ndani yake kuna furaha ya duniani na Akhera. Na miongoni mwake ni kwamba kujilazimisha kwake pamoja na kwamba hampendi ndani yake kuna kupigana dhidi ya nafsi na kuwa na maadili mazuri. Na huenda chuki hiyo ikaisha, na upendo ukachukua nafasi yake, kama ulivyo uhakika wa mambo katika hilo. Na huenda akapewa mtoto mwema kutoka kwake, akawanufaisha wazazi wake katika dunia na Akhera.