An-Nisaa
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِۦ ۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسْتَنكَفُوا۟ وَٱسْتَكْبَرُوا۟ فَيُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا 173
{173} Kisha akaeleza kwa kina hukumu yake kuhusiana nao, akasema, "Basi wale walioamini na wakatenda mema." Yaani, waliiunganisha kati ya imani iliyoamrishwa na kutenda mema, miongoni mwa wajibu mbalimbali na yaliyopendekezwa katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. "Atawalipa ujira wao kikamilifu," yaani malipo ambayo aliyaweka juu ya matendo kila mmoja kulingana na Imani yake na vitendo vyake. "Na atawazidishia katika fadhila yake," miongoni mwa malipo ambayo matendo hayakuchuma, wala vitendo vyao havikuyafikia, wala hayakuwaingia nyoyoni mwao. Na iliingia katika hilo kila kitu kilicho ndani ya Pepo miongoni mwa vyakula, na vinywaji, na mambo ya ndoa, na mambo ya kutazama, na furaha, na starehe ya moyo na roho, na starehe ya ya mwili. Bali inaingia katika hilo kila heri ya kidini na ya kidunia iliyowekwa juu ya imani na matendo mema. "Na ama wale waliojiinua juu, na wakafanya kiburi,"yaani, kuhusiana na kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, "basi atawaadhibu adhabu chungu." Nayo ni hasira ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu yake, na Moto uliookwa ambao utaingia nyoyoni. "Wala hawajitapa kando na Mwenyezi Mungu rafiki mwandani wala wa kuwanusuru." Yaani, hawatapata yeyote miongoni mwa viumbe atakayewafanya kuwa marafiki ili wafikie wanayoyataka, wala hata wa kuwanusuru ili awazuie kutokana na yale yenye kuogopwa. Bali aliwaachilia mbali Mwingi wa rehema, na akawaacha katika adhabu yao wadumu humo. Na kile alichohukumu Yeye Mtukufu, basi hakuna mwenye kurudisha hukumu yake, wala mwenye kubadilisha majaaliwa yake.