An-Nisaa
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
تِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ ۚ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدْخِلْهُ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ 13
{13} Yani, hayo maelezo aliyoyataja katika mirathi ni mipaka ya Mwenyezi Mungu ambayo ni lazima kusimama nayo, na kutoipita wala kuipunguza. Na katika hilo kuna ushahidi kwamba kumfanyia wasia mrithi kulibatilishwa kwa kukadiria kwake Yeye Mtukufu mafungu ya warithi. Kisha Yeye Mtukufu akasema, "Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiipite." Kwa hivyo, wasia kwa mrithi kwa kuzidisha haki yake unaingia katika huku kupita mipaka, pamoja na kauli yake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake; - "Hakuna wasia kwa mrithi." Kisha akataja kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuwaasi kwa ujumla. Ili iingie katika ujumla huo kushikamana na mipaka yake katika mirathi au kuacha hilo. Akasema, "Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake" kwa kutekeleza amri yao ambayo kubwa yake kabisa ni kumtii katika Tauhidi, kisha maamrisho kulingana na daraja zake tofauti tofauti. Na kujiepusha na makatazo yao ambayo ni makubwa yake zaidi ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kisha maasia kulingana na viwango vyake tofauti tofauti. "Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito chini yake, wadumu humo." Kwa hivyo, mwenye kutekeleza maamrisho na akaepuka makatazo, basi ni lazima aingie Peponi na kuokoka na Moto. "Na huko ndiko kufuzu kukubwa;" ambako kupitia huko alipata kuokoka kutokana na ghadhabu yake na adhabu yake, na kupata malipo yake na radhi zake za kufikia neema ya milele ambayo waelezaji hawawezi kuielezea.