Faatir
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَمَا يَسْتَوِى ٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْبَصِيرُ 19 وَلَا ٱلظُّلُمَـٰتُ وَلَا ٱلنُّورُ 20 وَلَا ٱلظِّلُّ وَلَا ٱلْحَرُورُ 21 وَمَا يَسْتَوِى ٱلْأَحْيَآءُ وَلَا ٱلْأَمْوَٰتُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَآءُ ۖ وَمَآ أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِى ٱلْقُبُورِ 22 إِنْ أَنتَ إِلَّا نَذِيرٌ 23
{19 - 23} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuwa vinyume si sawa katika hekima ya Mwenyezi Mungu, na katika yale aliyoyaweka katika maumbile ya waja wake. Kwa hivyo "kipofu halingani" "na anayeona wala giza na nuru, wala kivuli na joto. Wala hawalingani waliohai na maiti." Basi kama vile ilivyokwisha julikana vyema kwenu bila shaka yoyote ya kwamba hivi vilivyotajwa si sawa. Vivyo hivyo, jueni kwamba inafailia zaidi kutolingana vinyume viwili katika vitu visivyo vya kishisia. Kwa hivyo, Muumini na kafiri hawawi sawa, wala aliyeongoka na mpotofu, wala mwanazuoni na mjinga, wala watu wa Peponi na watu wa Motoni, wala waliohai moyoni na waliokufa humo. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mambo haya ambazo hazijui vilivyo isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu. Basi ukishajua viwango na ukapambanua mambo mbalimbali, na kinachopaswa kushindana ili kukipata kikawa wazi mbali na kinyume chake, basi mtu mwenye azimio kubwa na ajichagulie mwenyewe kilicho bora zaidi kwake na kinachostahili zaidi kupendelewa. "Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye" kusikia kwa kufahamu na kukubali. Kwani Yeye Mtukufu ndiye mwenye kuongoa na kuwezesha. "Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini;" yaani, wafu moyoni mwao. Au kama vile dua yako haiwanufaishi walio makaburini, vivyo hivyo haimnufaishi mwenye kupeana mgongo, mkaidi. Bali kazi yako ni kuonya tu na kufikisha uliyotumwa nayo. Sawa yatakubaliwa au yasikubaliwe, na ndiyo maana akasema: "Hukuwa wewe isipokuwa ni mwonyaji."