An-Naml
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
قِيلَ لَهَا ٱدْخُلِى ٱلصَّرْحَ ۖ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا ۚ قَالَ إِنَّهُۥ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ ۗ قَالَتْ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَـٰنَ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ 44
{44} Kisha Suleiman akataka kwamba (Malkia) aone katika mamlaka yake kile kinachoshangaza akili, kwa hivyo akamwamuru aingie kwenye behewa, ambalo ni baraza lililoinuka na ni pana, nalo lilikuwa baraza la sakafu ya vioo, ambalo mito inapita chini yake. "Akaambiwa: Liingie behewa la jumba hili. Alipoliona, alidhani ni maji," kwa sababu vioo ni wazi, na yanaonekana maji ambayo yako chini yake, kana kwamba hayo yenyewe ndiyo yanapita bila ya kuwepo kitu juu yake. "Na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake" ili aingie ndani yake. Na hili pia ni katika akili yake nzuri na adabu yake nzuri; kwa sababu hakukataa kuingia pale alipoamrishwa kuingia kwa sababu alijua kwamba hakuitwa isipokuwa kwa ajili ya kufanyiwa ukarimu, na kwamba ufalme wa Suleiman na mpangilio wake umejengeka kwa hekima, na wala hakukuwa na shaka yoyote moyoni mwake kutokea hali yoyote mbaya baada ya kuona kile alichokiona. Basi alipojiandaa kuingia humo, akaambiwa "Hakika hilo ni behewa liliosakafiwa kwa vioo!" Kwa hivyo, hakuna haja ya kuinua vazi juu ya miundi yako. Na alipofika kwa Suleiman na akaona kile alichokiona na akajua kwamba yeye ni nabii na Mtume, akatubia na akaachana na ukafiri wake, na "Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu, na sasa ninanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote." Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotusimulia katika kisa cha Malkia wa Sabai na kile kilichomtokea alipokuwa pamoja na Suleiman. Na chochote kisichokuwa hayo miongoni mwa matawi waliyozua watu, na hadithi Wana wa Israili, hayo hayawezi kutumiwa katika kutafsiri maneno ya Mwenyezi Mungu. Nayo ni katika mambo ambayo ili kuwa na uhakika juu yake kunahitaji kuwepo ushahidi unaojulikana usiokuwa na makosa. Lakini mambo yaliyosimuliwa katika mlango huu, yote au mengi yake siyo hivyo. Kwa hivyo mtu ajitahadharishe na ajiepushe nayo, na asiyaingize katika tafsiri. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.