Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِۦ ۚ وَقَالُوا۟ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ ٱلْمَصِيرُ 285 لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا ٱكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَآ إِن نَّسِينَآ أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَآ إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦ ۖ وَٱعْفُ عَنَّا وَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَآ ۚ أَنتَ مَوْلَىٰنَا فَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ 286
{285-286} Ilithibiti kutoka kwake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwamba, mwenye kuzisoma Aya mbili hizi usiku, zitamtosheleza. Yani kutokana na shari zote. Na hilo ni kwa sababu ya yale iliyojumuisha katika maana kubwa. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu aliwaamrisha watu mwanzoni mwa sura hii kumwamini Mwenyezi Mungu kwa misingi yake yote katika kauli yake. "Semeni: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale yaliyoteremshwa kwetu." Na akajulisha katika Aya hii kwamba Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na wale walio pamoja naye miongoni mwa Waumini waliiamini misingi hii mikubwa na Mitume wote na Vitabu vyote. Na hawakufanya kitendo cha wale walioamini baadhi na wakakufuru baadhi yake, kama hali ya wale wapotofu katika watu wa dini potofu. Na katika kuwaunganisha Waumini pamoja na Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – na kujulisha kuwahusu wote kwa habari moja ni heshima kubwa kwa Waumini. Na ndani yake kuna kwamba, yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - anawashiriki umma huu katika kumlenga na mazungumzo ya kisheria, na kuitekeleza kwake kamili. Na kwamba yeye amewapita Waumini, bali amewapita Mitume wote kwa kuisimamia imani na haki zake. Na kauli yake, "na wakasema: Tumesikia na tumetii". Ahadi hii ya Waumini ni ya jumla kwa yale yote aliyoyaleta Nabii, -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - katika Kitabu na Sunna. Na kwamba waliisikia kusikia kwa kukubali, kusalimu amri na kufuata. Na madhumuni ya hayo ni kunyenyekea kwao kwa Mwenyezi Mungu katika kuomba msaada wa kufanya hivyo. Na kwamba Mwenyezi Mungu atawasamehe yale waliyopungukiwa katika majukumu, na waliyoyafanya ya haramu. Na vile walimnyenyekea Mwenyezi Mungu katika dua hizi zenye manufaa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikwisha jibu dua yao kwa ulimi wa Nabii wake, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema, “Nimeshafanya.” Kwa hivyo, dua hizi zinakubaliwa kutoka kwa Waumini wote bila ya shaka. Na kutoka kwa kila mmoja wao binafsi, ikiwa hakuna kizuizi kwa hilo kutoka kwa mtu binafsi. Na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaondolea kuwachukulia ubaya katika kukosea na kusahau. Na kwamba Mwenyezi Mungu aliifanya sheria yake kuwa nyepesi sana kwao, na wala hakuwatwika katika uzito, dhiki, na minyororo aliyowatwika wale waliokuwa kabla yao. Na hakuwabebesha zaidi ya uwezo wao, na alikwisha wasamehe na akawarehemu na akawapa ushindi dhidi ya kaumu ya makafiri. Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa majina yake na sifa zake. Na kwa yale aliyotuneemesha kwayo ya kushikamana na dini yake, kwamba atufanikishie hayo. Na atutimizie yale aliyotuahidi kwa ulimi wa Nabii wake, na kwamba atengeneze hali za Waumini. Na inachukuliwa kutokana na hili msingi wa kurahisisha, na kukanusha ugumu katika mambo yote ya dini. Na msingi wa kufutilia mbali mabaya yaliyotokana na kusahau na kukosea katika ibada na katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na vile vile katika haki za viumbe katika upande wa kuondoa dhambi na kukashifiwa. Na ama kuhusu wajibu wa kudhamini uharibifu uliotokea kimakosa au kwa kusahau katika nafsi na mali, hilo linaingia katika kuharibu bila ya haki. Na hilo linajumuisha hali ya kukosea, kusahau na kukusudia. Imetimia tafsiri ya Surat Al-Baqara, na kuhimidiwa na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad.