Aller au contenu
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sourate 2

Al-Baqara

Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.

Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22

Verset 275

ٱلَّذِينَ يَأْكُلُونَ ٱلرِّبَوٰا۟ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِى يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيْطَـٰنُ مِنَ ٱلْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوٓا۟ إِنَّمَا ٱلْبَيْعُ مِثْلُ ٱلرِّبَوٰا۟ ۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلْبَيْعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰا۟ ۚ فَمَن جَآءَهُۥ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُۥ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ 275

{275} Mwenyezi Mungu alipoitaja hali ya watoao, na heri walizo nazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na namna anavyowafutia katika dhambi na makosa. Akawataja madhalimu, watu wa riba na biashara mbaya, na akajulisha kuwa watalipwa kulingana na matendo yao. Basi kama walivyokuwa katika dunia wakitafuta mapato mabaya kama wendawazimu, wakaadhibiwa katika makaburi na siku ya Kiyama. Kwamba hawatasimama kutoka makaburini mwao mpaka siku ya kufufuliwa kwao na kutawanyika kwao. "Isipokuwa kama anavyosimama aliyezugwa na Shetani kwa kumgusa," yani kutokana na uwendawazimu na kifafa. Na hiyo ni adhabu, na hizaya, na fedheha kwao, na kuwalipa juu ya riba yao na kudhihirisha kwao kwa kauli yao. "Hakika, biashara ni kama riba tu." Basi wakajumuisha - pamoja na ujasiri wao - baina ya aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, na wakaruhusu riba kwa hilo. Kisha Mola Mtukufu akawawekea toba wale wanaoamiliana na riba na wengineo, akasema: "Basi mwenye kujiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi," na huku ni kubainisha kulikoambatana na ahadi na tishio. "Kisha akakomeka" na yale aliyokuwa akichukua katika riba, "basi yake ni yaliyokwisha pita" katika yale aliyoyafanyia ujasiri. Kisha akatubia akayaacha "na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu" katika siku zake zijazo. Ikiwa ataendelea na toba yake hiyo, basi Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mema. "Na wenye kurudia" baada ya kubainisha kwa Mwenyezi Mungu, na kumkumbusha kwake, na kumuonya kwake mwenye kula riba; "basi hao ndio wenza wa Moto, wao watadumu humo." Katika hili kuna kwamba riba inalazimu (mtu) kuingia Motoni na kudumu humo. Na hilo ni kwa sababu ya ubaya wake maadamu hajazuiwa kudumu humo na kuzuizi cha imani. Na hii ni miongoni mwa hukumu zinazotegemea kuwepo kwa masharti yake na kutokuwepo kwa vizuizi vyake. Na hakuna hoja ndani yake ya Khawarij kama maandiko mengineyo ya vitishio. Kwa hivyo, la lazima ni kusadiki maandiko yote ya Kitabu na Sunna. Kwa hivyo, mja anaamini yale yaliyokuja katika maandishi yasiyo na shaka, kuhusu kutoka kwa Motoni kwa yule ambaye; ndani ya moyo wake kuna uzito mdogo zaidi wa chembe ya haradali wa imani. Na kuhusu kustahiki mwenye kuyafanya madhambi yaangamizayo haya yanayomlazimu kuingia Motoni ikiwa hatatubu kutokana nayo.