Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَإِذَا طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا۟ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُۥ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوٓا۟ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ هُزُوًا ۚ وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَمَآ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَٱلْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِۦ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ 231
{231} Kisha Yeye Mtukufu akasema, "Na mtakapowataliki wanawake" yani talaka ya kurejeleana bila ya nikaha mpya, kama vile talaka moja au mbili. "Nao wakafikia kumaliza muda wao (wa eda)" yani muda wakakaribia kumaliza muda wao wa eda. "Basi washikilieni kwa wema au waachilieni kwa wema." Yani ima muwarudishe hali ya kuwa nia zenu ni kuwatimizia haki zao, au muwaache bila ya kuwarudisha wala kuwadhuru. Na ndio maana akasema, "wala msiwashikilie kwa kuwadhuru, ili mkiuke mipaka" katika kufanya kwenu halali kuwa haramu. Kwani halali ni kushikilia kwa wema, nayo haramu ni kuwadhuru. "Na mwenye kufanya hilo, basi kwa hakika ameidhulumu nafsi yake." Na hata kama haki ni ya kiumbe, lakini madhara yanamrudia yule aliyetaka kufanya madhara, "wala msizifanyie Aya za Mwenyezi Mungu mzaha". Mwenyezi Mungu alipoibainisha mipaka yake kwa uwazi kabisa, na yakawa makusudio ni kuijua, kuifanyia kazi, kusimama nayo, na kutoikiuka, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuibainisha bure. Bali aliiteremsha kwa haki, ukweli, na kuipa uzito mkubwa. Kwa hivyo, akakataza kuifanyia mzaha, yani kuifanyia mchezo kwa kuiasi na kutotekeleza wajibu wake, kama vile: Kukusudia madhara katika kumshikilia mke (aliyetalikiwa), au kuachana naye, au kutaliki kwa wingi, au kufanya talaka tatu kwa pamoja. Ilhali Mwenyezi Mungu katika rehema yake alimfanyia talaka mmoja baada ya nyingine kwa sababu ya kufanyia upole na kutaka kumtekelezea masilahi yake. "Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu" kwa ujumla, kwa kuhimidi na kusifu kwa ulimi. Na kwa kukubali na kukiri kwa moyo, na kwa viungo kwa kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu. "Na yale aliyowateremshia katika Kitabu na hekima," yani Sunna ambayo kwa mawili hayo aliwabainishia njia za heri; na akawahimiza juu yake. Na njia za shari, na akawatahadharisha dhidi yake. Na akajijulisha kwenu, na matukio yake katika marafiki wake na maadui zake, na akawafundisha yale ambayo hamkuwa mnayajua. Na ilisemwa kuwa kinachokusudiwa ni hekima ni siri za Sheria. Kwa sababu, Kitabu kina hukumu, nayo hekima ina ufafanuzi wa hekima ya Mwenyezi Mungu katika maamrisho yake na makatazo yake. Na kila maana mbili hizi ni sahihi. Na ndio maana akasema, "anayowawaidhi kwayo." Yani kwa yale aliyoyateremsha juu yenu. Na hili ni katika yale yenye kutilia nguvu kuwa kilichokusudiwa na hekima ni siri za sheria. Kwa sababu, mawaidha ni kubainisha hukumu na hekima, na kutia moyo au kutishia. Kwa hivyo, kuhukumu kwayo kunaondoa ujinga. Nayo hekima pamoja na kutia moyo yanasababisha mtu kuwa na moyo katika jambo. Nayo hekima pamoja na kutishia yanasababisha hofu "na mcheni Mwenyezi Mungu" katika mambo yenu yote. "Na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu." Ndio maana akawabainishia hukumu hizi kwa ukamilifu wa hali ya juu na zaidi, na hukumu ambazo zinakwendana na masilahi (ya watu) katika kila wakati na mahali. Kwa hivyo, sifa njema zote na wema ni vyake.