Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أُو۟لَـٰٓئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ ٱللَّهِ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 218
{218} Matendo haya matatu ndiyo kichwa cha furaha na nguzo ya uja, na kwalo yanajulikana yale ambayo mtu anayo ya faida na hasara. Ama imani, basi usiulize juu ya fadhila zake. Na vipi utauliza kuhusu kitu ambacho ndicho kitenganishi cha watu wa furaha na watu wa taabuni, na watu wa Peponi na watu wa Motoni? Nayo ndiyo ambayo ikiwa pamoja na mja, matendo mema hukubaliwa kutoka kwake. Na isipokuwa naye, haitakubaliwa kwake kikomboleo wala toba, wala faradhi wala sunna. Na ama kuhama, huku ni kujitenga yale yanayopendwa na mtu na yaliyozoeleka, kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo, mwenye kuhama anaiacha nchi yake, mali zake, familia yake na marafiki zake, ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kunusuru dini yake. Na ama jihadi, hii ni kufanya juhudi katika kupigana vita na maadui, na kujitahidi kikamilifu kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, na kukomesha dini ya Shetani. Kwa hivyo, atakayetelekeza matendo haya matatu licha ya dhiki zake na ugumu wake, basi atakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuzifanya matendo mengineyo kwa ukamilifu. Basi, hawa wanafaa zaidi kwamba wao ndio wanaotarajia rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, walileta sababu inayoleta rehema. Na katika hili kuna ushahidi kwamba matarajio hayawezi kuwepo isipokuwa baada ya kutimiza sababu za furaha. Na ama matarajio yanayofungamana na uvivu, na kutofanya sababu, hilo ni kutoweza, kutamani tu na kudanganyika. Na hilo linaashiria udhaifu wa hima ya mwenyewe, na upungufu wa akili yake, kama mtu anayetarajia kupata mtoto bila ya kuoa; na kupatikana kwa mavuno bila ya mbegu wala kumwagilia maji, na mfano wa hayo. Na katika kauli yake, “hao ndio wanaotarajia rehema za Mwenyezi Mungu;” kuna ishara ya kwamba mja hata akitenda atendayo katika matendo, hafai kuyategemea, na kutaka msaada wake. Bali anafaa kutarajia rehema za Mola wake Mlezi, na anatarajia kukubaliwa kwa matendo yake, na kusamehewa dhambi zake, na kufunikiwa kasoro zake. Ndiyo maana akasema: “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe.” Yani kwa anayetubia toba ya kweli, “Mwenye kurehemu” ambaye rehema zake zimeenea kila kitu, na ukarimu wake na hisani yake vimejumuisha kila kilicho hai. Na katika hili, kuna ushahidi kwamba yeyote anayefanya haya matendo yaliyotajwa, atapata msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa maana, mema huondoa maovu, na anapata rehema za Mwenyezi Mungu. Na ikipata msamaha, basi zinamwondokea adhabu za duniani na Akhera, ambazo ni athari za dhambi ambazo zimeshasamehewa na athari zake zikaondoka. Na akipata rehema, atapata kila heri duniani na Akhera. Bali matendo yao yaliyotajwa ni kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na lau kuwa sio kuwafanikisha kwake, wasingeyataka. Na lau kuwa si kuwapa kwake uwezo juu ya yake, basi wasingeweza kuyafanya. Na lau kuwa si hisani yake, basi wasingeyakamilisha na akayakubali kutoka kwao. Basi, fadhila zote ni zake mwanzoni na mwishoni. Naye ndiye aliyeweka bure sababu na matokeo yake. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: