Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا۟ فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَآ أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَـٰتٍ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ عِندَ ٱلْمَشْعَرِ ٱلْحَرَامِ ۖ وَٱذْكُرُوهُ كَمَا هَدَىٰكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِۦ لَمِنَ ٱلضَّآلِّينَ 198
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamrisha uchamungu, alijulisha Yeye Mtukufu kwamba kutafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa kuchuma katika misimu ya Hija na mingineyo, hakuna ubaya wowote; ikiwa hakutashughulisha na yale ambayo ni ya lazima ikiwa lengo ni kuhiji. Na yakawa hayo mapato ni halali yanayohusishwa na fadhila ya Mwenyezi Mungu, siyo yenye kunasibishwa na ustadi wa mja, na kutegemea sababu tu na kumsahau mwenye kusababisha. Basi huo ndiyo ubaya wenyewe. Na katika kauli yake :“Basi mtakapomiminika kutoka 'Arafat, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril Haram (eneo takatifu).” Kuna dalili ya mambo: La kwanza: Kusimama ‘Arafa, na kwamba ilikuwa inajulikana kuwa ni nguzo katika nguzo za Hijja. Kwa maana, kumiminika kutoka ‘Arafa hakuwi isipokuwa baada ya kusimama ‘Arafa. La pili: Amri ya kumtaja Mwenyezi Mungu katika Mash’aril Haram, napo ni Muzdalifah. Na hili pia ni maarufu. Analala usiku wa kuamkia (siku ya) kuchinja hapo. Na baada ya swalah ya Alfajiri, atasimama Muzdalifah akiomba dua, mpaka kuangaze sana. Na anaingia katika kumtaja Mwenyezi Mungu hapo, akitekeleza sala za faradhi na za sunna hapo. La tatu: Kusimama Muzdalifah kuko nyuma ya kusimama ‘Arafah, kama inavyoonyeshwa na neno ‘kisha’ na utaratibu (uliopo katika vitendo vya aya). La nne na la tano: Kwamba ‘Arafa na Muzdalifah zote ni katika maeneo takatifu ya Hija yanayokusudiwa kufanywa na kudhihirishwa. La sita: Kwamba Muzdalifah iko katika Haram (eneo takatifu), kama alivyoifunganisha na neno ‘takatifu’. La saba: Kwamba ‘Arafa iko katika eneo lisilokuwa takatifu (Al-Hill), kama inavyofahamika katika maana isiyokuwa ya moja kwa moja katika kufunganisha Muzdalifah na neno ‘takatifu’. “Na mtajeni kama alivyowaongoa, ijapo kabla ya hilo mlikuwa miongoni mwa waliopotea.” Yani mtajeni Mwenyezi Mungu Mtukufu kama alivyowaneemesha kwa uwongofu baada ya upotovu, na kama alivyowafundisha yale ambayo hamkuwa mnayajua. Na hii ni katika neema kubwa mno ambazo kuu ni lazima kuzishukuru na kuzikabili kwa kumtaja aliyeneemesha kwa moyo na ulimi.