Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَلَمَّا جَآءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ كِتَـٰبَ ٱللَّهِ وَرَآءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ 101
(101) Yani alipowajia Mtume huyu mtukufu na Kitabu kitukufu kwa haki inayokubaliana na waliyo nayo. Na walikuwa wakidai kuwa wao wameshikamana na Kitabu chao. Na walipomkufuru Mtume huyu na yale aliyokuja nayo, "kundi moja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu hicho" ambacho kiliteremshwa juu yao. Yani walikitupa kwa kukikataa "nyuma ya migongo yao." Na huku ndiko kupeana mgongo kwa juu mno, kana kwamba wao katika kitendo chao hiki ni wajinga, hali ya kuwa wanajua ukweli wake na uhakika wa yale aliyokuja nayo. Inabainika kwa hili kwamba kundi hili la Watu wa Kitabu halikubaki na chochote katika mikono yao, kwa vile hawakumuamini Mtume huyu. Basi, kukawa kumkufuru kwao ni kukikufuru kitabu chao bila ya kutambua. Na pindi ilipokuwa miongoni mwa marejeo ya majaaliwa na hekima ya Mwenyezi Mungu ni kwamba, mwenye kuacha yale yanayomnufaisha hali ya kuwa anaweza kunufaika nayo, na asifaidike nayo; anapewa mtihani wa kujishughulisha na yenye kumdhuru. Kwa hivyo, mwenye kuacha kumuabudu Arrahman (Mwingi wa Rehema); anapewa mtihani wa kuabudu masanamu. Na mwenye kuacha kumpenda Mwenyezi Mungu, kumhofu na kumtumaini; anapewa mtihani wa kupenda asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kumhofu, na kumtumaini. Na yule asiyetumia mali yake katika kumtii Mwenyezi Mungu, ataitumia katika kumtii Shetani. Na mwenye kuacha kumdhalilikia Mola wake Mlezi; anapewa mtihani wa kuwadhalilikia waja. Na mwenye kuiacha haki; anajaribiwa na batili (uongo).