Aller au contenu
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
Sourate 16

An-Nahl

Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.

Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22

Verset 89

وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِى كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ ۚ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ تِبْيَـٰنًا لِّكُلِّ شَىْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ 89

{89} Alipotaja hapo katika yaliyotangulia kwamba atatoa shahidi katika kila umma, pia akataja hilo hapa, na akamtaja miongoni mwa Nabii huyu mtukufu tu. Akasema, "na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa" yaani, juu ya umma wako, ukiwashuhudia ya heri na maovu. Na hili ni katika ukamilifu wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwamba kila Mtume anashuhudia juu ya umma wake. kwa sababu yeye ndiye ajuaye zaidi matendo ya umma wake kuliko wengineo, na aliye mwadilifu zaidi na mwenye huruma zaidi kiasi kwamba hawezi kushuhudia juu yao isipokuwa kile wanachostahili. Na hii ni kama kauli yake yeye Mtukufu, "Na vivyo hivyo tumewafanya muwe Umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu." Na amesema yeye Mtukufu, "Basi itakuwa vipi tutakapoleta kutoka kwa kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi dhidi ya hawa? Siku hiyo watapenda wale waliokufuru na wakamuasi Mtume lau kuwa ardhi isawazishwe kwa wao." Na kuali yake, "Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu" kuhusiana na misingi ya dini na matawi yake, na kuhusiana na hukumu za nyumba hizi mbili, na kila kitu ambacho waja wanahitaji, basi kimeelezwa humo kwa ufafanuzi kamili, na kwa maneno yaliyo wazi na maana za wazi kabisa, kiasi kwamba yeye Mtukufu anarudia humo mambo makubwa ambayo moyo unahitaji kuyapitia kila wakati na kuyarudia kila saa. Na anayaonyesha kwa maneno tofauti tofauti na ushahidi anuai ili yakae mioyoni na kuzalisha heri na wema kulingana na uthabiti wake moyoni, na tena kiasi kwamba Yeye Mtukufu anaunganisha katika maneno machache yaliyo wazi, maana nyingi, basi yakawa maneno hayo ndiyo kanuni na msingi wake. Na lizingatie hili katika aya inayofuata aya hii, na aina mbalimbali za amri na makatazo zilizo ndani yake ambazo haziwezi kuwekewa mipaka. Na wakati Qur-ani hii ilipokuwa ni ufafanuzi wa kila kitu, ikawa ni hoja ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake wote, kwa hivyo hoja ya madhalimu ikakatika kwa hilo, na Waislamu wakafaidika nayo, kwa hivyo ikawa ni uwongofu kwao ambao wanaongoka kwayo katika mambo ya dini yao na dunia yao, na ni rehema ambayo wanapata kwayo kila heri katika dunia hii na Akhera. Na uwongofu ni kile walichopata kutokana na elimu yenye manufaa na matendo mema. Nayo rehema ni matokeo ya hayo miongoni mwa malipo ya dunia na Akhera, kama vile kutengenea kwa moyo, na wema wake, utulivu wake, na ukamilifu wa akili ambao hautimii isipokuwa tu kwa kuilea juu ya maana zake ambazo ndizo maana tukufu zaidi na za juu kabisa. Na rehema hiyo pia katika matendo matukufu, maadili mema, riziki pana, nusura dhidi ya maadui kwa maneno na matendo, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na utukufu wake mkubwa ambao hajui neema ya kudumu iliyomo isipokuwa Mola Mlezi, mwingi wa kurehemu.