Hud
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
قَالُوا۟ يَـٰشُعَيْبُ أَصَلَوٰتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ ءَابَآؤُنَآ أَوْ أَن نَّفْعَلَ فِىٓ أَمْوَٰلِنَا مَا نَشَـٰٓؤُا۟ ۖ إِنَّكَ لَأَنتَ ٱلْحَلِيمُ ٱلرَّشِيدُ 87
{87} "Wakasema: Ewe Shua'ibu! Je, ni sala zako ndizo zinazokuamrisha tuyaache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu?" Yaani, walisema hayo kwa njia ya kumkejeli Nabii wao na kulifanya kuwa mbali sana jambo la kuitikia kwa Nabii wao. Na maana ya maneno yao hayo ni kwamba, hakuna sababu ya wewe kukataza haya isipokuwa kwamba wewe unaswali na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, ukiwa hivyo, je, inatulazimu kuyaacha yale waliokuwa baba zetu wakiwaabudu kwa sababu tu ya kauli ambayo hakuna ushahidi wowote juu yake isipokuwa tu kwamba inaafikiana nawe? Basi vipi tukufuate na kuwaacha baba zetu wa kale wenye akili na ufahamu? Na vile vile kauli yako hiyo haitulazimu kufanya katika mali zetu yale uliyotuambia ya kutimiza vipimo na mizani, na kutekeleza haki za wajibu ndani yake. Bali hatutaacha kuendelea kufanya ndani yake chochote tunachotaka. Kwa sababu hizo ni mali zetu, nawe huna uendeshaji wowote ndani yake. Basi ndiyo maana wakasema katika kejeli zao: "hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu mno!" Yaani, je, wewe ndiye yule ambaye ustahamilivu na heshima ni katika tabia zako, na uongofu ndiyo mwenendo wako? Basi hakitoki kwako isipokuwa uwongofu tu, wala huamrishi isipokuwa uwongofu tu, na wala hukatazi isipokuwa upotovu? Yaani, mambo siyo hivyo na wanachomaanisha ni kwamba yeye anasifika kwa kinyume cha sifa hizi mbili: upumbavu na upotovu. Na maana yake ni kwamba, vipi utakuwa wewe ndiye mstahamilivu zaidi, mwongofu na baba zetu wawe ndio wapumbavu na wapotofu? Na kauli hii waliyoisema kwa mbinu ya kejeli, na kwamba mambo yake ni kinyume chake, si kama walivyodhania. Bali mambo yake ni kama walivyosema kwamba Swalah yake inamuamrisha awakataze yale waliyokuwa wakiabudu baba zao wapotofu na kwamba wafanye katika mali zao watakavyo. Kwa maana, Swala inakataza uchafu na maovu na ni uchafu upi na uovu ulio mkubwa zaidi kuliko kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kuliko kuzuia haki za waja wa Mwenyezi Mungu, au kuziiba kwa vipimo na mizani, na bila shaka yeye - rehema na amani ziwe juu yake - ndiye mstahamilivu zaidi, mwongofu zaidi?