پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Lail
سورهٔ ۹۲

Al-Lail

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۱۷–۲۱

وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلْأَتْقَى ۱۷ ٱلَّذِى يُؤْتِى مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ ۱۸ وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰٓ ۱۹ إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِ ٱلْأَعْلَىٰ ۲۰ وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ۲۱

{17 - 21} "Na mcha Mungu ataepushwa nao. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa." Naye ni yule ambaye huifanya nia yake kwa hilo ni kujitakasa na kutokana na madhambi na uchafu, tena kwa kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hili linaonyesha kwamba ikiwa kutoa matumizi yaliyopendekezwa kunajumuisha kuacha wajibu kama vile deni, kutoa matumizi ya wajibu na mfano wake; basi hilo haliruhusiwi. Bali kutoa kwake huko kunakataliwa kulingana na na wanachuoni wengi. Kwa sababu hawezi kujitakasa kwa kufanya jambo linalopendekezwa ambalo litamfanya akose jambo la faradhi. "Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndio anamlipa." Pia na inaweza kuwa na maana ya kwamba hakuna yeyote aliye na cha kumdai huyu mcha Mungu isipokuwa tayari ashamlipa juu yake, na hata huenda fadhila zake fulani zilibakia juu ya watu, kwa hivyo akawa ni mja aliyesafika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Na ama yule ambaye anapaswa kuwalipa watu kitu fulani, na bado hajawalipa, basi ni lazima awaachie watu na awafanyie mambo ambayo yatapunguza uaminifu wake kwa Mwenyezi Mungu. Ingawa Aya hii inamjumuisha Abu Bakr As-Siddiq, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, bali hata imesemwa kwamba iliteremka kwa sababu yake. Kwani, yeye Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, hakuwa na neema ya mtu juu yake aliyopaswa kuilipa, hata Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- isipokuwa neema ya Mtume ambayo haiwezi kulipwa, nayo ni neema ya kumlingania kwenye dini ya Kiislamu na kumfundisha uongofu na dini ya haki. Kwani Mwenyezi Mungu na Mtume wake wana neema juu ya kila mtu, neema isiyoweza kulipwa wala kulinganishwa. Kwani inajumuisha kila mwenye kusifika kwa sifa hizi adhimu. Kwa hivyo, hakuna hata mmoja katika viumbe aliyebakisha neema yake juu yake inayopasa kulipwa, basi matendo yake yakabakia kuwa safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo maana akasema: "Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. Naye atakuja ridhika" huyu mcha Mungu zaidi kwa aina za neema na mambo matukufu ambayo Mwenyezi Mungu anampa.

Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.