پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورهٔ ۹

At-Tawba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۷۱

وَٱلْمُؤْمِنُونَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ ٱللَّهُ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ۷۱

{71} Alipotaja kuwa wanafiki wanatokana wao kwa wao, akataja kwamba Waumini ni marafiki walinzi wao kwa wao, akawasifu kwa kinyume cha alichowasifu kwacho wanafiki, kwa hivyo akasema: "Na Waumini wanaume na Waumini wanawake;" yaani, wa kiume wao na wa kike wao "wao kwa wao ni marafiki walinzi;" katika mapenzi, na kushirikiana, na kufungamana, na kunusuriana. "Huamrisha mema." Nalo ni jina linalojumuisha kila linalojulikana kuwa ni heri miongoni mwa itikadi mbalimbali nzuri, na matendo mema, na maadili mema, na watu wa kwanza anayeingia katika amri yao ni wao wenyewe. "Na hukataza maovu." Nayo ni kila kitu kinachopingana na mema, na kuyapunguza miongoni mwa itikadi batili, na matendo maovu, na tabia chafu, "Na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake." Yaani hawajaacha kushikamana na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake daima. "Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu;" yaani, atawaingiza katika rehema yake na kuwazunguka kwa ihsani yake. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yaani, ni Mwenye nguvu, Mshindi. Lakini pamoja na nguvu zake, Yeye ni Mwenye hekima, anakiweka kila kitu pahali pake panapokistahili, ambaye anasifiwa kwa alichokiumba na alichoamrisha.