At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلَوْ أَرَادُوا۟ ٱلْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا۟ لَهُۥ عُدَّةً وَلَـٰكِن كَرِهَ ٱللَّهُ ٱنۢبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ ٱقْعُدُوا۟ مَعَ ٱلْقَـٰعِدِينَ ۴۶
{46} Yeye Mtukufu anasema akibainisha kwamba wale waliosalia nyuma miongoni mwa wanafiki tayari ulikwisha tokea kwao ushahidi unaoonyesha kwamba hawakukusudia kutoka kabisa, na kwamba visingizio vyao walivyotoa ni batili. Kwa maana Udhuru ni kile kizuizi kinachozuia ikiwa mja atafanya uwezo wake na kujitahidi kutafuta sababu za kutoka, kisha kizuizi cha kisheria kikamzuia. Basi huyu ndiye aliyekubaliwa udhuru wake. "Na" ama wanafiki hawa , kama kweli "wangelitaka kweli kutoka, basi bila ya shaka wangelikuandalia maandalizi." Yaani, wangejitayarisha na kufanya wawezayo miongoni mwa sababu, lakini wakati hawakujitayarisha kwa ajili yake matayarisho ya kweli, ikajulikana ya kuwa hawakutaka kutoka. "Lakini Mwenyezi Mungu alichukia kutoka kwao" pamoja nanyi kwenda katika vita, "kwa hivyo akawazuia" kimajaliwa na kihukumu hata ingawa aliwaamrisha na akawahimiza juu ya kutoka na akawafanya kuwa na uwezo juu yake. Lakini kwa hekima yake, hakutaka kuwasaidia, bali aliwachilia mbali na akawazuia, "na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa!" Miongoni mwa wanawake na wale waliokubaliwa udhuru wao.