پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورهٔ ۹

At-Tawba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۳۸

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ٱنفِرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱثَّاقَلْتُمْ إِلَى ٱلْأَرْضِ ۚ أَرَضِيتُم بِٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا مِنَ ٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ فَمَا مَتَـٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ ۳۸

Kisha Yeye Mtukufu akasema:

{38} Jua ya kwamba sehemu nyingi za Sura hii tukufu ziliteremka kuhusiana na Vita vya Tabuk, wakati Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipowaita Waislamu waende kupigana na Warumi, na wakati huo ulikuwa wa joto, na chakula cha safarini kilikuwa kichache, na maisha yalikuwa magumu. Kwa hivyo, baadhi ya Waislamu wakapatwa na uzito ambao ulisababisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwalaumu juu ya hilo na kuwahimiza wanyanyuke. Kwa hivyo akasema Yeye Mtukufu: "Enyi mlioamini:" Je, hamtendi kwa matakwa ya imani na mahitaji ya yakini kama vile kuiendea haraka amri ya Mwenyezi Mungu, na kukimbilia kumridhisha, na kufanya jihadi dhidi ya maadui zake, na kuinusuru dini yenu? Basi "Mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?" Yaani mnakuwa wavivu na mnageuka kuelekea katika ardhi na starehe, na utulivu humo. "Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera?" Yaani, hali yenu siyo isipokuwa ni kama hali ya yule aliyetosheka na dunia hii na akaifanyia juhudi na kutojali akhera. Na ni kana kwamba hakuiamini. "Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na Akhera" ambazo ziliwageuza na mkazitanguliza mbele ya Akhera "isipokuwa chache." Je, Mwenyezi Mungu hakuwapa akili mnazoweza kupima nazo mambo? Ni kwamba ni yapi yake yanastahiki zaidi kupendelewa? Je, si dunia hii tangu mwanzo wake hadi mwisho wake haina ulinganisho wowote katika Akhera? Na ni kipimo gani cha umri wa mtu kilicho kifupi sana katika dunia hii ambacho anakifanya kuwa ndilo lengo ambalo hakuna lengo lingine zaidi yake, ndiyo afanye juhudi zake, na taabu zake, na wasiwasi wake, na kutaka kwake, hazidi maisha haya mafupi ya dunia hii, yaliyojaa shida na yaliyobeba hatari nyingi? Basi je, ni kwa maoni gani mliona kuipendelea kuliko Nyumba ya Akhera, inayokusanya kila neema, ambayo ndani yake kuna yale yanayotamaniwa na nafsi, na macho yanayafurahia, na nyinyi mtadumu humo? Basi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba haipendelei dunia kuliko akhera yule ambaye imani iliingia ndani ya moyo wake, wala ambaye maoni yake ni mazuri, wala mwenye kuhesabiwa kuwa miongoni mwa wenye akili.