پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورهٔ ۹

At-Tawba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۳۱

ٱتَّخَذُوٓا۟ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَـٰنَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَٱلْمَسِيحَ ٱبْنَ مَرْيَمَ وَمَآ أُمِرُوٓا۟ إِلَّا لِيَعْبُدُوٓا۟ إِلَـٰهًا وَٰحِدًا ۖ لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ عَمَّا يُشْرِكُونَ ۳۱

{31} Na ilikuwa hivyo, ijapokuwa linashangaza kwa umma mkubwa, mwingi kwamba wakubaliane juu ya kauli ambayo kunaonyesha ubatili wake kutafakari kudogo na kuweka akili juu yake. Kwa kuwa, hilo lina sababu. Nayo ni kwamba wao "walichukua makuhani wao," nao ni wanazuoni wao “na wamonaki wao;” yaani, wale wafanyao ibada ambao walijitoa kwa ajili ya kufanya ibada tu, "mabwana badala ya Mwenyezi Mungu." Wanawahalalishia yale ambayo Mwenyezi Mungu aliharimisha, nao wanayahalalisha pia. Na wanawaharamishia yale ambayo Mwenyezi Mungu alihalalisha, nao pia wanayaharamisha. Na wanatungia sheria na maneno yaliyo kinyume na dini ya Mitume, nao wanawafuata katika hayo, na wanawatukuza, na wanayafanya makaburi yao kuwa masanamu yanayoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Wanayakusudia kwa dhabihu, na dua, na kuomba msaada. “Na pia Masihi bin Maryam” walimfanya kuwa mungu badala ya Mwenyezi Mungu. Na hali ni kwamba walikiuka katika hilo amri ya Mwenyezi Mungu kwao kwa juu ya ndimi za Mitume wake. Kwani kilichoamrisha tu ni kuabudu Mungu mmoja; “hawakuamrishwa isipokuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hakuna mungu isipokuwa Yeye.” Kwa hivyo wamuabudu yeye tu na kutii, na wampende yeye peke yake, na wamfanyie yeye tu dua. Lakini wakaitupa amri ya Mwenyezi Mungu, na wakashirikisha na yale ambayo hakuteremsha hoja yoyote juu yake. “Ametakasika” na ametukuka “na hayo wanayomshirikisha nayo.” Yaani, amesafika, na ametakasika, na umetukuka ukuu wake kutokana na shirki yao na uzushi wao. Kwa sababu wao wanampunguzia hadhi kwa hayo, na wanamsifu kwa yale yasiyoufailia utukufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu, ni wa juu zaidi katika sifa zake, na matendo yake kutokana na yote ambayo yalimhusisha nayo miongoni mwa yale yanayopingana na ukamilifu wake mtakatifu.