پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورهٔ ۹

At-Tawba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۹

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ ٱلْحَآجِّ وَعِمَارَةَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ كَمَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَجَـٰهَدَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ لَا يَسْتَوُۥنَ عِندَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ۱۹

{19} Wakati baadhi ya Waislamu au baadhi ya Waislamu na baadhi ya washirikina walipotofautiana katika kupendelea kuuimarisha Msikiti Mtakatifu kwa kuujenga, na kusali, na kufanya ibada ndani yake, na kuwanywesha maji mahujaji kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu na kufanya jihadi katika njia Yake, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha tofauti iliyo kati yao. Kwa hivyo akasema: "Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji;" yaani, kuwanywesha maji kutoka Zamzam, kama inavyojulikana kama jina hili linapotumiwa bila ya kufungiwa kwamba hilo ndilo linalokusudiwa, "na kuimarisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akafanya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa kwa Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo kufanya Jihadi na kumwamini Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko kuwanywesha maji mahujaji na kuuimarisha Msikiti Mtakatifu kwa daraja nyingi. Kwa maana, imani ndio msingi wa Dini, na kwayo ndiyo matendo yanakubaliwa na sifa zinatakasika. Na ama kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi ndiyo kilele cha nundu ya Dini, [ambayo] kwayo dini ya Kiislamu huhifadhi na kupanuliwa, na inanusuriwa haki, na inaangushwa batili. Na ama kuuimarisha Msikiti Mtukufu na kuwanywesha maji mahujaji, basi hayo hata kama ni matendo mema, hayo yanategemea imani, na hayana masilahi kama yaliyo katika imani na kufanya jihadi. Na ndiyo maana akasema, "Hawawi sawa kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu dhalimu." Yaani, wale ambao sifa yao ni dhuluma, ambao hakiwafailii kukubali kitu chochote cha wema, bali haiwafailii isipokuwa uovu tu.