At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَلَا تُقَـٰتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوٓا۟ أَيْمَـٰنَهُمْ وَهَمُّوا۟ بِإِخْرَاجِ ٱلرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ أَتَخْشَوْنَهُمْ ۚ فَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۱۳
{13} Kisha akawahimiza kupigana nao na akawachochea Waumini kwa kutaja sifa ambazo zilitokea kwa maadui hawa, na ambazo wanasifiwa kwazo, zinazohitaji kupigana vita nao. Kwa hivyo akasema: "Je, hampigani na kaumu waliovunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumtoa Mtume" ambaye ni lazima kumheshimu, na kumfanyia taadhima, na kumtukuza, na walitaka sana kumfurusha na kumtoa katika nchi yake, na waliwania mno katika hilo wawezavyo, "nao ndio waliowaanza mara ya kwanza" kwa kuwa walivunja maagano, na wakawasaidia wengine dhidi yenu. Na hilo ni wakati Maquraishi ambao walikuwa katika agano na Bani Bakr walipowasaidia washirika wao wandani dhidi ya Khuza'a, washirika wandani wa Mtume wa Allah rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na wakapigana pamoja nao kama ilivyoelezwa kwa urefu katika Sira ya Mtume. "Je, mnawaogopa?" katika kuacha kupigana nao? "Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini." Kwani Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kupigana nao, na akasisitiza hilo juu yenu kusisitiza kukubwa zaidi. Kwa hivyo ikiwa nyinyi ni Waumini, basi fuateni amri ya Mwenyezi Mungu, wala msiwahofu, mkaacha amri ya Mwenyezi Mungu.