At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَءَاخَرُونَ ٱعْتَرَفُوا۟ بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا۟ عَمَلًا صَـٰلِحًا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ۱۰۲
{102} Yeye Mtukufu Anasema: "Na wengine" miongoni mwa wale walio Madina na walio pembezoni mwake, bali hata katika nchi zote za Kiislamu, “walikiri dhambi zao.” Yaani, walikiri na wakajuta juu yake, na wakajitahidi kuyatubia na kujitakasa na uchafu wake "walichanganya matendo mema na mengine mabaya.” Na matendo hayawi mema isipokuwa ikiwa mja ana msingi wa Tauhidi na imani yenye kutoa katika ukafiri, na ushirikina ambao ndilo sharti la kila jambo jema. Basi hawa walichanganya matendo mema na mabaya, kama vile kuwania kufanya baadhi ya mambo yaliyoharamishwa na kutofanya baadhi ya majukumu, huku wakikiri hilo na kutaraji kuwa Mwenyezi Mungu atawasamehe. Hawa ndio "huenda Mwenyezi Mungu akakubali toba zao.” Na kukubali kwake toba ya mja wake ni kwa aina mbili: Ya kwanza ni kumwezeha kutubia. Na ya pili ni kuikubali baada ya yeye kutubia. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” Yaani, sifa yake kusamehe na kurehemu, ambayo hakuna kiumbe yeyote asiyekosa hayo. Bali ulimwengu wa juu na wa chini hauwezi kubakia isipokuwa kwa hayo. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angewaadhibu watu kwa dhuluma yao, basi hangeliacha juu ya mgongo wake mnyama yeyote, “hakika, Mwenyezi Mungu ndiye anayezizuia mbingu na ardhi zisiondoke. Na lau kuwa zingeondoka, basi hakuna yeyote wa kuzizuia isipokuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole, Mwenye kusamehe.” Na katika msamaha wake ni kwamba wale waliozidhulumu nafsi zao na wakakata umri wao kwa matendo maovu, ikiwa watatubia kwake na wakarejea, hata kama ni karibu na mauti yao kwa muda mfupi sana, Yeye hakika anawasamehe na kuachilia mbali matendo yao mabaya. Basi Aya hii inaashiria kwamba mwenye kuchanganya mazuri na maovu, mwenye kukiri, mwenye kujuta, ambaye hakutubu toba ya kweli, kwamba yeye yuko chini ya hofu na matumaini, na yuko karibu zaidi na usalama. Na ama mwenye kuchanganya mema na maovu, ambaye hakukiri, wala hajutii juu ya yale aliyoyafanya kabla, bali bado anadumu katika dhambi, basi yeye anahofiwa kuhofiwa kukubwa.