As-Saff
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِى وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّى رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيْكُمْ ۖ فَلَمَّا زَاغُوٓا۟ أَزَاغَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ ۵
{5} Yaani, “Na Musa alipowaambia watu wake” akiwakemea kwa vitendo vyao na kuwakaripia kwa sababu ya kumudhi kwao ilhali wanajua kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. “Kwa nini mnaniudhi” kwa maneno na vitendo “nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliyetumwa kwenu?” Na Mtume ana haki ya kuheshimiwa na kupewa taadhima, na kutekeleza amri zake na kuharakisha kushika hukumu zake. Na kumdhuru Mtume ambaye wema wake kwa viumbe uko juu ya wema wote baada ya wema wa Mwenyezi Mungu, hilo ni katika dhuluma kubwa zaidi, ujasiri dhidi yake, kukengeuka na kupotea mbali na njia iliyonyooka, ambayo waliijua na wakaiacha, na ndiyo maana akasema: “Walipokengeuka” wakaiacha Haki makusudi, “Mwenyezi Mungu akazipotoa nyoyo zao” ili iwe ni adhabu ya kukengeuka kwao huko walikokuchagua wenyewe na wakakuridhia, na Mwenyezi Mungu hakuwawezesha kufikia uwongofu. Kwa sababu hawafailii wema na wala hawafailii isipokuwa uovu tu. “Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wavukao mipaka” ambao hiyo ndiyo sifa yao na wala hawana nia ya kuongoka. Aya hii tukufu inaashiria kwamba Mwenyezi Mungu kuwapotoa waja wake si dhuluma kwa upande wake wala si udhuru kwao dhidi yake. Bali hilo ni wao waliojisababishia wenyewe. Kwani wao wenyewe ndio waliojifungia mlango wa uwongofu baada ya kuutambua, na baada ya hayo akawalipa kwa upotofu, kukengeuka, na kubadilisha nyoyo, ili iwe ni adhabu kwao na kuwafanyia uadilifu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyokuwa hawakuiamini mara ya kwanza, kisha tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga.”