As-Saff
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ ۲ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ ٱللَّهِ أَن تَقُولُوا۟ مَا لَا تَفْعَلُونَ ۳
{2 - 3} “Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?” Yaani, kwa nini mnasema ya heri na mkahimiza juu yake, na pengine mnasifu wengine kwa sababu yake ilhali nyinyi wenyewe hamuifanyi, na mnakataza maovu, na pengine mkajifanya kwamba mnajiweka mbali nayo ilhali mnasifika na kujichafua kwayo? Je, hali hii ya kukashifiwa inawafailia waumini? Au ni katika chukizo kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu mja kusema asichofanya? Kwa ajili hiyo, mwenye kuamrisha mema na awe mtu wa kwanza kuharakisha kuifanya. Na mwenye kukataza maovu na awe mbali zaidi nayo kuliko watu wote. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Je, mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamtumii akili?” Na Nabii Shuaib, amani iwe juu yake, alisema [akiwaambia watu wake]: “Wala mimi sipendi kukuhalifuni nikafanya yale ninayokukatazeni.”