Al-Mumtahana
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلْيَوْمَ ٱلْـَٔاخِرَ ۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ ۶
{6} Kisha akarudia kuwahimiza kuwaiga na akasema: “Kwa yakini umekuwa mfano mzuri kwenu katika mwendo wao.” Lakini mfano huu si rahisi kwa kila mtu, bali ni rahisi kwa wale “anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho” kwani imani na kutaraji malipo mazuri humrahisishia mja kila lililo gumu, na linampunguzia kila kilicho kingi, na linamsababishia kuzidisha kuwaiga waja wema wa Mwenyezi Mungu, Manabii na Mitume. Kwani anajiona kuwa anahitaji na kulazimika sana kufanya hivyo, “Na mwenye kugeuka” akaacha kumtii Mwenyezi Mungu na kuwafuata Mitume wa Mwenyezi Mungu, basi hatamdhuru yeyote ila nafsi yake mwenyewe, na wala hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, “Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha” mwenye kujitosheleza kikamilifu katika kila jambo, na wala hahitaji kiumbe chake chochote. “Msifiwa mno” katika dhati yake, [majina yake], sifa zake, na vitendo vyake. Yeye anasifiwa kwa yote hayo.