پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
سورهٔ ۶

Al-An'aam

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۹۱

وَمَا قَدَرُوا۟ ٱللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِۦٓ إِذْ قَالُوا۟ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَىْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ ٱلْكِتَـٰبَ ٱلَّذِى جَآءَ بِهِۦ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُۥ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوٓا۟ أَنتُمْ وَلَآ ءَابَآؤُكُمْ ۖ قُلِ ٱللَّهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِى خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ۹۱

{91} Haya ni kuonyesha ubaya wa yule ambaye aliukataa jumbe miongoni wa Mayahudi na washirikina, na akadai kuwa Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote kwa mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, mwenye kusema haya, basi hajamheshimu mwenyezi Mungu haki ya kumheshimu, wala hakumtukuza haki ya kumtukuza. Kwa maana, haya ni kuitusi hekima yake, na ni madai kwamba anawaacha waja wake bila ya kuwajali. Wala hawaamrishi wala hawakatazi, na ni kuikanusha neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwayo waja wake, ambayo ni ujumbe ambao hakuna njia kwa waja ya kupata furaha, na utukufu, na kufaulu isipokuwa kwa njia hiyo. Basi ni tusi gani kwa Mwenyezi Mungu lililo kubwa zaidi ya hili? "Sema," uwaambie huku ukiwalazimu kukubali ubovu wa maneno yao, na wafanye kukiri kwa yale wanayoyakiri. "Ni nani aliyekiteremsha Kitabu alichokuja nacho Musa?" Nacho ni Taurati tukufu, "huku ikiwa nuru" katika giza mbalimbali ya ujinga, "na uwongofu;" kutoka katika upotovu, na chenye kuongoa kwenye njia iliyonyooka kwa elimu na vitendo, nacho ni Kitabu ambacho kilienea na kutangazika na utajo wake ukajaa nyoyoni na masikioni, mpaka wakawa wanakiandika katika nyaraka, na kukifanyia kama wanavyotaka. Basi Chochote kinachoafikiana na matamanio yao kwacho, wanakionyesha na kukidhihirisha. Na chochote chenye kuhalifu hilo, wanakificha, na hayo ni mengi. "Na mkafundishwa" katika elimu mbalimbali ambazo ni kutokana na Kitabu hicho kitukufu "yale mliyokuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu?" Basi ukiwauliza kuhusu ni nani aliyekiteremsha Kitabu hiki kilichoelezwa kwa sifa hizi; basi jibu swali hili na "Sema: Mwenyezi Mungu" ndiye aliyekiteremsha. Na hapo ukweli utakuwa wazi, na kudhihirika kama jua, na hoja itasimama juu yao. "Kisha" ukishawalazimisha kulazimisha huku, "waache wacheze katika porojo lao;" Yaani, waache waingie kwenye batili na wacheze na yale yasiyokuwa na faida mpaka wakutane na siku yao ambayo wanaahidiwa.