پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
سورهٔ ۶

Al-An'aam

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۷۱

قُلْ أَنَدْعُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰٓ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ كَٱلَّذِى ٱسْتَهْوَتْهُ ٱلشَّيَـٰطِينُ فِى ٱلْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُۥٓ أَصْحَـٰبٌ يَدْعُونَهُۥٓ إِلَى ٱلْهُدَى ٱئْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ۷۱

{71} "Sema" ewe Mtume, kuwaambia wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, ambao wanawaomba wengine pamoja naye, wale wanaowalinginia nyinyi katika Dini yao, ukiwabainishia na kufafanua sifa za miungu yao, ambayo anazuilika mwenye akili timamu kwa kuitaja tu badala ya kumkataza juu yao. Kwa maana, kila mwenye akili timamu anapolitafakari dhehebu la washirikina, anakuwa na uhakika juu ya ubatili wake kabla kusimamishwa hoja dhidi yake. Kwa hivyo akasema, "Je, tumwombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatufai wala hatudhuru?" Na ni maelezo yanayojumuisha kila anayeabudiwa badala ya mwenyezi Mungu. Hanufaishi wala hadhuru, na wala hana kitu chochote katika jambo hilo. Jambo hilo ni la Mwenyezi Mungu tu. "Na turejeshwe nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuongoa?" Yaani, tugeuke baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoa, tukaenda katika upotovu, na kutoka kwenye njia iliyonyooka kwenda kwenye upotofu, na kutoka kwenye njia inayofikisha kwenye mabustani ya neema na kuelekea kwenye njia ziendazo kwenye adhabu chungu! Basi hii ni hali ambayo hakuna mtu mwenye akili timamu anayeiridhia, na mwenye hali hii ni “kama yule ambaye mashetani wamempumbaza katika ardhi?” Yaani, walimpotoa na wakampoteza kutoka kwenye njia yake na mwongozo wake unaomfikisha kwenye makusudio yake, kwa hivyo akabaki “amechanganyikiwa? Anao wenza wanaomwita aende kwenye uwongofu” nao mashetani wanamwita kwenye maangamio, kwa hivyo akabakia amechanganyikiwa kati ya wawili hao wanaomwita. Na hii ndiyo hali ya watu wote, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu amemlinda. Wao kwa hakika wanapata ndani yao vivutio na sababu zinazopingana. Mwenye kuitaka kwenye Ujumbe na, akili sahihi, timamu, na umbile la asili lililonyooka anamwita kwenye uwongofu na kupanda hadi daraja za juu zaidi, na waitaji wa Shetani na mwenye kufuatao njia yake, na nafsi iamrishayo maovu wanamwita kwenye upotevu na kuteremka hadi kiwango cha chini kuliko walio chini. Basi Miongoni mwa watu kuna yule ambaye anakuwa pamoja na walinganizi wa uwongofu katika mambo yake yote au mengi yake. Na miongoni mwao kuna yule ambaye ni kinyume cha huyu. na miongoni mwao kuna yule ambaye miito hii miwili ni sawa kwake, na mivuto hii miwili inapingana kwake; na katika maudhui haya kuna kuwajua watu wa furaha, na watu wa mashaka. Na kauli yake, "Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu;" yaani, uwongofu si chochote isipokuwa ile njia ambayo Mwenyezi Mungu ameiwekea sheria kwenye ulimi wa Mtume wake, na kisichokuwa hicho ni upotovu na maangamizo. "Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote;" kwa kufuata kumpwekesha yeye na tusalimu amri yake na makatazo yake na tuingie katika [kundi la] uja wake. Kwa maana hii ndiyo neema bora zaidi ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwayo waja wake, na malezi kamili zaidi aliyowafikishia.