Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَ جَنَّـٰتٍ مَّعْرُوشَـٰتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَـٰتٍ وَٱلنَّخْلَ وَٱلزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيْتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَـٰبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَـٰبِهٍ ۚ كُلُوا۟ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثْمَرَ وَءَاتُوا۟ حَقَّهُۥ يَوْمَ حَصَادِهِۦ ۖ وَلَا تُسْرِفُوٓا۟ ۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلْمُسْرِفِينَ ۱۴۱
{141} Yeye Mungu Mtukufu alipotaja matendo ya washirikina katika mengi ya yale aliyowahalalishia Mwenyezi Mungu miongoni mwa mimea na mifugo, yeye Mwingi wa baraka, Mtukufu akataja neema yake juu yao katika kwa hayo na majukumu yao ya wajibu juu yao katika mimea na mifugo hao, kwa hivyo akasema: "Na Yeye ndiye aliyeziumba mabustani." Yaani, mabustani yenye aina mbalimbali za miti na mimea tofautitofauti, "yenye kutambaa kwenye fito." Yaani, baadhi ya mabustani hayo yamefanyiwa fito ambazo juu yake inatambaa miti na kuisaidia kuinuka juu kutoka juu ya ardhini, na baadhi yake haina fito inayomea juu yake, lakini ina mashina au inajitandaza kwenye ardhi. Na katika hii kuna tanabahisho juu ya wingi wa manufaa zake na heri zake, na kwamba yeye Mtukufu aliwafundisha waja wake jinsi ya kuitia kwenye fito na kuikuza. "Na" yeye Mtukufu alianzisha "mitende na mimea yenye vyakula mbalimbali." Yaani, yote iko mahali pamoja, na inakunywa katika maji moja, na Mwenyezi Mungu hupendelea baadhi yake kuliko mingine katika vyakula. Na yeye Mtukufu aliufanya mtende kuwa maalumu na mimea kwa aina zake tofautitofauti kwa sababu ya wingi wa manufaa yake na kwa kuwa hiyo ndicho chakula kikuu cha wengi wa viumbe. "Na" yeye akaanzisha "mizaituni na mikomamanga inayofanana" katika miti yake, "na isiyofanana" katika matunda yake na ladha yake. Na ni kana kwamba ilisemwa: kwa nini yeye Mtukufu alianzisha mabustani haya? Na ni nini alichofungamanisha nayo? Basi akajulisha kwamba aliyaanzisha kwa sababu ya manufaa ya waja wake, na akasema: "Kuleni katika matunda yake;" yaani, mitende na mimea, "inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake." Yaani, toeni haki ya mazao hayo, ambayo ni Zaka yenye mafungu yaliyopimwa katika sheria. Aliwaamuru waitoe siku ya kuvunwa kwake. Na hilo ni kwa sababu mavuno ya mazao ni sawa na kupita kwa mwaka. Kwa sababu ndio wakati ambao nafsi za masikini huyatazamia, na ni rahisi kwa wenye mazao kuyatoa, na jambo hili wakati huo linakuwa dhahiri kwa mwenye kuitoa, ili apambauke mwenye kuitoa na yule asiyeitoa. Na kauli yake: "Wala msitumie kwa kupitiliza" inajumuisha katazo la kupitiliza katika kula. Nako ni kupitiliza kiwango. Na amekataza kwamba mwenye mazao hayo ale kula kwenye kuidhuru Zaka. Na kupitiliza katika kutoa haki ya mazao ni kwamba atoe zaidi ya kile wajibu ulioko juu yake, au ajidhuru mwenyewe, au familia yake, au wadai wake. Yote haya ni katika kupitiliza ambako Mwenyezi Mungu alikataza, ambako Mwenyezi Mungu hakupendi, bali anakuchukia, na anachukia sana. Na katika Aya hii kuna ushahidi wa ulazima wa Zaka katika matunda, na kwamba hakuna ulazima wa kupita mwaka mmoja, bali muda wake ni kwa kuvunwa kwake katika mazao na kuichuma mitende, na kwamba Zaka haitajirudia katika hayo ikiwa yatabaki kwa mja kwa miaka mingi ikiwa si kwa ajili ya biashara. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hakuamrisha itolewe humo ila wakati wa mavuno yake. Na ikiwa janga liliyapata kabla ya hapo bila ya kupuuza kwa mwenye mazao hayo na matunda, ni kwamba hayadhamini, na kwamba inaruhusika kula katika mitende na mazao kabla ya kutoa humo Zaka, na kwamba hilo halihesabiwi katika Zaka, bali atatoa Zaka katika mali iliyobaki baada yake. Na Nabii - sala za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie – alikuwa akimtuma mwenye kukadiria ili awakadirie watu matunda yao, na anamwamuru awaachie wenyewe theluthi moja au robo kulingana na yanayokuwa humo ya kula na mengineyo, wenyewe na wengineo.