پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Mujaadila
سورهٔ ۵۸

Al-Mujaadila

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱

قَدْ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوْلَ ٱلَّتِى تُجَـٰدِلُكَ فِى زَوْجِهَا وَتَشْتَكِىٓ إِلَى ٱللَّهِ وَٱللَّهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَآ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌۢ بَصِيرٌ ۱

{1} Aya hizi tukufu ziliteremshwa kwa sababu ya mwanamume mmoja kutoka kwa answari ambaye mke wake alimlalamikia Mwenyezi Mungu na akamjadili mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, baada ya mume wake kujiharamishia mke huyu baada ya kuishi pamoja naye kwa muda mrefu na kupata watoto. Mume huyo alikuwa ni mzee sana, kwa hivyo mke wake akamlalamikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuhusu hali yake na hali ya mume wake, na akalirudia hilo sana. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha sikia usemi wa mwanamke anayejadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno." Anasikia zaidi sauti zote katika nyakati zote, hata pamoja na kutofautiana kwa mahitaji. "Mwenye kuona zaidi." Anamuana sisimizi mweusi, juu ya jiwe jeusi, katika usiku wa giza totoro. Huku ni kupeana habari kuhusu ukamilifu wa kusikia kwake na kuona kwake, na kudhibiti kwake sawasawa mambo ya madogo mno (ya siri mno) na makubwa pia, na ndani ya hayo kuna ishara kwamba Mwenyezi Mungu [Mtukufu] atamwondolea malalamiko yake na kutoa balaa yake. Ndiyo maana akataja hukumu yake na hukumu ya wanawake wengineo kwa ujumla, akasema: