Al-Waaqia
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ ۸۸ فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ ۸۹
{88 - 89} Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja hali za makundi haya matatu: walio karibu na Mwenyezi Mungu, wale wa mkono wa kulia, na wale wanaokadhibisha, wapotofu, pale mwanzoni mwa sura hii watakapokuwa katika nyumba ya kukaa milele, kisha akataja hali zao mwishoni mwake wakati wa kufa kwao, akasema: "Kwa hivyo, akiwa miongoni mwa wale walio karibu na Mwenyezi Mungu." Anayejiweka karibu naye kwa kutekeleza faradhi na mambo yasiyo ya faradhi, na kuacha maharamisho na mambo yanayochukiza na mambo madogo madogo yanayoruhusiwa, "Basi" kwao itakuwa "ni raha" utulivu, furaha na bashasha za moyo na roho "na manukato." Pia ilisemekana kwamba maana ya 'rayhan' hapa ni jina linalojumuisha kila aina ya starehe za kimwili kwa aina zote za vyakula, vinywaji na mengineyo. Na pia ilisemekana kwamba 'rayhan' ni manukato yale yale yanayojulikana, na hii inakuwa ni katika mbinu za kutumia kitu fulani kuwakilisha aina zake zote, "na Bustani zenye neema" ambazo ndani yake yamo yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia na wala hayajawahi kupitia katika moyo wa mwanadamu yeyeote. Basi wale walio karibu na Mwenyezi Mungu hupewa habari njema wakati wa kifo, ambazo kwa sababu yake roho zinakaribia mno kuruka nje kwa furaha na bashasha. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika wale waliosema: 'Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu!' Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: 'Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa bustani ya mbinguni mliyokuwa mkiahidiwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka. Ni karamu ya kuwakaribisha itokayo kwa Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu zaidi." Na kauli yake [Mwenye baraka tele] aliyetukuka: "Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera" ilifasiriwa kwamba bishara hii iliyotajwa ndiyo bishara watakayopewa katika maisha ya dunia hii.