Qaaf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَّقَدْ كُنتَ فِى غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلْيَوْمَ حَدِيدٌ ۲۲
{22} Jambo hili ni katika mambo lazima mja ayakumbuke kila mara, lakini watu wengi wameghafilika, na ndiyo maana akasema: "(Aambiwe), 'Kwa hakika ulikuwa umeghafilika mbali na haya.'" Yaani, maneno haya ataambiwa Siku ya Kiyama huyu mwenye kupeana mgongo na kukadhibisha kwa njia ya kumkaripia, kumlaumu na kumkemea sana. "Basi" sasa "leo tumekuondolea pazia lako" lililokuwa limefunika moyo wako, kwa hivyo usingizi wako ukawa mwingi na ukaendelea kupeana mgongo. "Na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali mno." Atayaona yenye kumsumbua na kumuogopesha miongoni mwa adhabu na mateso. Au haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu akimwambia mja wake. Kwani duniani alikuwa ameghafilika mbali na aliyoumbwa kwa ajili yake, lakini siku ya Kiyama atakuwa macho sana, na usingizi wake utamwondoka katika wakati ambapo hatoweza kurekebisha yale ambayo hakuyafanya vyema wala kufanya yaliyompita. Yote hayo ni kuhofisha anakowahofisha Mwenyezi Mungu waja wake, na ni kuwatishia kwa kutaja yale yatakayowapata wale wanaokadhibisha katika siku hiyo kuu.