Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَـٰقَهُ ٱلَّذِى وَاثَقَكُم بِهِۦٓ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ۷
{7} Mwenyezi Mungu anawaamrisha waja wake kukumbuka neema zake za kidini na za kidunia kwa nyoyo zao na ndimi zao. Kwani katika kuendelea kuzikumbuka linasababisha kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumpenda na kuujaza moyo na wema wake. Na ndani yake kuna kuondoa kujiona na neema za kidini na kuongezeka kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na wema wake "na agano lake." Yaani, na kumbukeni agano lake "ambalo aliwafunga kwalo." Yaani, ahadi yake ambayo aliichukua juu yenu. Na siyo kwamba walitamka na kusema ahadi hiyo na agano hilo. Bali kinachokusudiwa kwa hilo, ni kwamba, kwa imani yao kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wanakuwa wameahidi kushikana na kuwatii wao. Na ndiyo maana akasema, "mliposema: Tumesikia na tumetii." Yaani, tumeyasikia yale uliyotulingania kwayo katika Aya zako za Qur-ani na za kiulimwengu, kusikia kwa kufahamu, na utiifu, na kufuata, na tumetii yale uliyotuamrisha kwa kuyatekeleza na uliyotukataza kwa kuyaepuka. Na hili linajumuisha Sheria zote za Dini zilizo dhahiri na zilizofichika. Na kwamba, Waumini wanakumbuka katika hilo ahadi ya Mwenyezi Mungu na agano lake juu yao, nayo yanakuwa katika akili zao, na wanafanya bidii katika kutekeleza yale waliyoamrishwa kwa ukamilifu bila ya kupunguza. "Na mcheni Mwenyezi Mungu" katika kila hali zenu. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua sana yaliyomo ndani ya vifua," yaani, yale yaliyomo ndani yake miongoni mwa mawazo, na siri, na fikira. Kwa hivyo, jihadharini asije kuona katika nyoyo zenu jambo asiloliridhia, au kitoke kwenu kile anachokichukia. Na ziimarisheni nyoyo zenu kwa kumjua Yeye, na kumpenda Yeye, na kuwanasihi waja Wake. basi Mkiwa hivyo, atawasamehe mabaya yenu na atawazidishia mazuri kwa sababu ya kujua kwake kutengenea kwa nyoyo zenu.