Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ وَأَكْلِهِمُ ٱلسُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ۶۲
{62} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaendelea kuhesabu makosa yao kwa kutetea dhidi ya kuwakashifu kwao waja Wake Waumini. Kwa hivyo akasema, "Na utawaona wengi miongoni mwao," yaani, miongoni mwa Mayahudi; "Wanakimbilia kwenye dhambi, na kupita mipaka." Yaani, wanawania na wanayaharakishia maasia yanayohusiana na haki za Muumba na kupita mipaka kuhusiana na viumbe. "Na ulaji wao vya haramu," na hakuachia kwa kujulisha tu kwamba wanayafanya hayo, mpaka akajulisha kwamba wanayakimbilia. Na hili linaashiria uchafu na uovu wao na kwamba nafsi zao zimefanywa kupenda maasia, na dhuluma. Na pamoja na hayo, wao wanajidai kuwa wako kwenye vyeo vya juu,; "Ni maovu mno hayo wayatendayo." Na hili ni kuwakashifu kwa hali ya juu sana, na kuwakosoa.