پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
سورهٔ ۵

Al-Maaida

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۵۵

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُمْ رَٰكِعُونَ ۵۵

{55} Alipokataza kuwafanya makafiri kuwa marafiki wandani miongoni mwa Mayahudi na Wakristo na wengineo, na akataja marejeo ya kuwafanya kuwa marafiki wandani kwamba ni hasara iliyo wazi. Yeye Mtukufu alijulisha kuhusu yale ambaye ni wajibu na ni yeye tu anapasa kumfanya kuwa rafiki mwandani, na akataja manufaa ya hayo na masilahi yake. Kwa hivyo akasema, "Hakika rafiki yenu mwandani ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake." Na urafiki wandani wa Mwenyezi Mungu unafikiwa kwa imani na uchamungu. Kwa hivyo kila aliye Muumini mchamungu; Mwenyezi Mungu anakuwa rafiki yake mwandani. Na yule ambaye ni rafiki mwandani wa Mwenyezi Mungu, basi yeye ni rafiki mwandani wa Mtume wake. Na mwenye kumfanya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa rafiki mwandani, inakuwa ukamilisho wa hilo ni yeye kumfanya rafiki mwandani yule anayemfanya Yeye Mwenyezi Mungu kuwa rafiki mwandani, ambao ni Waumini waliodumisha imani kwa nje na ndani. Na wakampwekesha muabudiwa wao kwa kusimamisha Swala kwa masharti yake, na faradhi zake, na yale yenye kuikamilisha, na wakawafanyia wema viumbe; na wakatoa Zaka katika mali zao kwa wale wanaoistahiki kutoka kwao. Na kauli yake "nao wanarukuu." Yaani, wanamnyenyekea Mwenyezi Mungu na kujidhalilisha mbele yake. Kwa hivyo, neno la kufungia katika kauli yake, "Hakika rafiki yenu mwandani ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini" linaashiria kwamba, ni lazima kuufungia urafiki wandani katika wale waliotajwa peke yao, na kujitenga na kuwafanya marafiki wandani wasiokuwa wao.