پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
سورهٔ ۵

Al-Maaida

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۵۰

أَفَحُكْمَ ٱلْجَـٰهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ ٱللَّهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ۵۰

{50} "Je, wanataka hukumu za Kijahiliya?" Yaani, Je, wanatafuta kwa kugeuka kwao na kukupa kwao mgongo hukumu ya Jahiliyyah? Nayo ni kila hukumu inayohalifiana na yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake. Basi hakuna isipokuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake au hukumu ya Jahiliyyah. Kwa hivyo, mwenye kuipa mgongo hiyo ya kwanza, atajaribiwa na hiyo ya pili, ambayo imejengeka juu ya ujinga, na dhulma na makosa. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaifungamanisha na ujinga. Na ama hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; hiyo imejengeka juu ya elimu, na uadilifu, na haki, na nuru, na uwongofu. "Na ni nani aliye mzuri zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?" Basi, mwenye yakini ni yule ambaye anajua kutofautisha kati ya hukumu mbili hizi, na kupambanua kwa yakini yake yale yaliyo katika hukumu ya Mwenyezi Mungu ya ubora na uzuri, na kwamba inabakia tu kiakili na kisheria kuifuata. Na yakini ni elimu kamili inayolazimu kutenda matendo.