پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
سورهٔ ۵

Al-Maaida

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴۵

وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَآ أَنَّ ٱلنَّفْسَ بِٱلنَّفْسِ وَٱلْعَيْنَ بِٱلْعَيْنِ وَٱلْأَنفَ بِٱلْأَنفِ وَٱلْأُذُنَ بِٱلْأُذُنِ وَٱلسِّنَّ بِٱلسِّنِّ وَٱلْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُۥ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ ۴۵

{45} Hukumu hizi ni miongoni mwa hukumu ambazo ziko katika Taurati, ambazo Manabii ambao waliojisalimisha, na wachamungu, na wanachuoni wa kiyahudi wanahukumu kwazo wale waliotubia na wakarudi (yani Mayahudi). Kwa maana Mwenyezi Mungu aliwawajibishia kwamba ikiwa nafsi itauawa, basi itauawa kwa sharti la kukusudia na kuwepo usawa. Na jicho linatolewa kwa jicho, na sikio linachukuliwa kwa sikio, na jino linang’olewa kwa jino. Na mfano wa hayo ni vile vilivyo mfano wake miongoni mwa viungo ambavyo inawezekana kutekeleza kisasi katika hivyo bila ya dhuluma. "Na kwa majeraha ni kisasi." Na kulipiza kisasi ni kwamba afanyiwe kama alivyofanya yeye. Basi mwenye kumjeruhi mwingine kwa makusudi, atalipizwa kisasi aliyejeruhi kwa kumtia jeraha mfano wa alivyomjeruhi yule aliyejeruhiwa kwa kiasi na mahali, na urefu, na upana, na kina. Na ifahamike kuwa sheria ya wale waliokuwa kabla yetu ni sheria yetu pia madamu sheria yetu haijaja na chenye kuihalifu. "Lakini mwenye kuitoa kama sadaka," yaani mwenye kuachilia mbali kulipiza kisasi katika nafsi na viungo na majeraha yaliyo chini yake, kwa kumsamehe aliyetenda kosa na ikamthibitikia haki juu yake, "basi hiyo ni kafara kwake;" yaani, kafara kwa aliyekosa. Kwa sababu mwanadamu aliiachilia mbali haki yake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kustahiki zaidi na kufailia zaidi kuisamehe haki yake. Na pia ni kafara kwa yule aliyesamehe, kwa kuwa kama vile alivyomsamehe yule aliyemfanyia uhalifu au mtu anayehusiana na uhalifu huo, basi Mwenyezi Mungu anamsamehe makosa yake na uhalifu wake. { Na yule asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu. Ibn Abbas alisema, hii ni kufuru chini ya kufuru kubwa, dhuluma chini ya dhuluma kubwa, na kupindukia mipaka chini ya kupindukia mipaka kukubwa. Basi ni ukafiri mkubwa ikiwa atahalalisha hilo, na ni dhambi kubwa ikiwa atalifanya bila ya kuamini kuwa ni halali kufanya hivyo.