Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ ۛ أَرْبَعِينَ سَنَةً ۛ يَتِيهُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ فَلَا تَأْسَ عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْفَـٰسِقِينَ ۲۶
{26} "Akasema" Mwenyezi Mungu akiitikia dua ya Musa, "Basi hakika nchi hiyo wameharimishiwa, kwa muda wa miaka arobaini watakuwa wakitangatanga katika ardhi." Yaani, hakika katika adhabu yao ni kuwa tunawaharamishia kuingia katika kijiji hiki ambacho [alikiandika] Mwenyezi Mungu [kwa ajili yao]; kwa muda wa miaka arobaini. Na katika muda huo pia watatangatanga katika ardhi bila kuongoka kupata njia wala hawatakaa wakatulia. Na hii ni adhabu ya kidunia. Huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwasitiria dhambi kwa hilo, na akawaondolea adhabu kubwa zaidi kuliko hiyo. Na hakika hili kuna ushahidi kwamba, adhabu juu ya dhambi inaweza kuwa ni kutoweka kwa neema iliyopo, au kuzuiwa neema iliyofungiwa kwa sababu ya kuwepo kwake ilithibitika, au kuahirishwa kwake mpaka wakati mwingine. Na pengine hekima katika kipindi hiki ni kwamba, wafe wengi wa hawa ambao walisema kauli hii iliyotoka katika mioyo isiyokuwa na subira wala uthabiti. Bali ilikwisha zoea kutumikishwa na adui yake, wala haina hamu zenye kuiinua kufikia kwenye kustawi kwake na kuinuka kwake, na ili kitokee kizazi kipya ambacho akili zake zinalelewa juu ya kutafuta kuwashinda maadui zao na kutotumikishwa, na kudhalilishwa vinavyozuia furaha. Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipojua kwamba mja wake Musa ni mwingi wa rehema kwa viumbe, hususan kaumu yake. Na kwamba huenda akawa mpole kwao na akabebwa na huruma kuwahuzunikia katika adhabu hii au kuwaombea iwaondokee, pamoja na kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha ipitisha. Kwa hivyo akasema, "Basi wewe usiwasikitikie watu wapotovu." Yaani, usiwaonee huruma wala usiwe na huzuni. Kwa maana wametoka nje ya mipaka, na kutoka kwao nje ya mipaka huko kulilazimu kutokea kwa yale yaliyowapata, si kwa sababu ya Sisi kuwadhulumu.